Tumekuwa tunasikia kila upandacho utavuna. Ni kweli ni sahihi kabisa. Ila jiulize hivi ukipanda mahindi shambani ukayaacha huko hadi wakati wa Mavuno utakutana na mahindi kiasi gani?

Ukiruka hatua ya Kuhudumia kile ulichokipanda basi tegemea kukuta mavuno hafifu.
Mchakato wa Kuhudumia ni mrefu na ndio huamua uvune kiasi gani katika kile ulichopanda.

Unajua hata mahusiano hayajengwi kwa kukutana na mtu siku moja lazima muendelee kuwasiliana kila wakati.

Kitu ninachoamini kuwa kinaweza kuota chenyewe bila ya kuhudumiwa ni magugu. Yale mambo Yasiyo na mchango chanya kwenye maisha yako wakati mwingine hata usipoyahudumia huleta matokeo yake. Ukidhulumu mara moja lazima tu itakuletea shida.

Sina maana unapomtendea mtu mema uendelee kumtendea au kuwa karibu nae hadi Ubarikiwe hapana bali usitende mema leo halafu ukae usubiri matokeo. Endelea kila siku kutenda mema na wewe utapokea mema isiyo na kikomo.

Ukitaka kufanikiwa kibiashara lazima ujifunze kuizalisha fedha na kuiongeza na sio kuiweka na kusubiri iongezeke yenyewe.

Jambo lolote unalolifanya ili lilete matokeo Kumbuka kuna mchakato ambao utasababisha matokeo. Kama huo mchakato unakuhitaji uwepo hakikisha unakuwepo kwasababu usipokuwepo unaweza usipate kile ulichokitarajia.

Uwe na Wiki Yenye Mafanikio Makubwa.
Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading