Kati ya glasi iliyo tupu na iliyojaa maji siku zote ile tupu ndio hupata nafasi ya kuwekewa maji mengine.

Watu wengi tunapenda Kuonekana tunajua kila kitu. Tunapenda Kuonekana sisi kuliko hata vile tunavyovifanya.

Ni muhimu ujue kuwa Unapokuwa kama glas tupu maana yake wewe ni mtu unaefanyia kazi yale ujifunzayo.

Huachi glasi ikiwa na maji bali unachukua hatua na kiu yako ya kutaka kujifunza inaongezeka.

Yafanyie kazi yale unayojifunza. Hujifunzi ili uje uoneshe wengine wewe unajua kuliko wao.

Unapokuwa Glasi iliyotupu unajiweka katika utayari wa kupokea vitu Vipya ndani yako.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.
www.jacobmushi.com/coach

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading