Chochote unachopitia kwenye maisha yako kama hakijayaondoa maisha yako basi kimekufanya uwe imara zaidi.
Tofauti ni kwamba kuna watu badala ya kuwa imara wanakuwa waoga.
Umeingia kwenye biashara ukapata hasara pesa zote zikapotea badala ya kuwa imara unakuwa muoga na hujaribu tena.
Unaingia kwenye mahusiano unaumizwa halafu inakuwa kama hutaki tena, na unaanza kusema wanaume/wanawake wote wanafanana. Unaogopa hata kuingia tena kwenye mahusiano. Huo ni udhaifu, Usikubali changamoto zikufanye uwe dhaifu na mwoga.
Hapana haitakiwi kuwa hivyo kama upo hai haijalishi Umepitia kwenye maumivu ya aina gani unapaswa kuwa imara zaidi.
Magumu unayopitia kwenye maisha yako ni kukufanya uwe imara zaidi.
Usikubali hata mara moja Kujiona hufai, huwezi, kwasababu tu Umeshindwa kwenye changamoto fulani.
Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.
www.jacobmushi.com/coach