Kuna watu huchanganya mafanikio na starehe. Unajua kuna tofauti kubwa sana kati ya kustarehe na mtu alie na amani ya moyo baada ya kufanya kile alichozaliwa kuja kufanya.


Mafanikio sio kuacha kazi na kukaa nyumbani kwasababu una pesa za kutosha.


Usipoteze maisha yako kufanya vitu ambavyo haviachi alama yeyote kwenye dunia hii na kwenye maisha ya wengine.


Hivo vitu unavyofurahia kutumia kuna watu waligundua jiulize kuna mtu anatumia changu?Kuna mtu anafurahia kazi ya mikono yangu?


Jiulize Swali hili rahisi sasa hivi na ulifanyie kazi. Unataka kitu gani watu wafurahie kutumia ambacho kimetoka kwenye akili zako? Kila mtu ana uwezo huo, nguo ulizovaa ni mtu aligundua, simu unayotumia, kitanda ulicholala leo, nyumba unayoishi, nyimbo unazosikiliza na kadhalika.
Wewe ni kipi binadamu wanafurahia hata kama ni kidogo?


Nakutakia Kila la Kheri.

Ubarikiwe sana.

Rafiki Yako Jacob Mushi.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading