Jaribu kuvuta picha sasa hivi, upo nyumbani kwenu na hali yako ya kimaisha ni ngumu. Mfukoni huna hata tsh elfu tano, ghafla unapokea simu kwamba maombi uliyowahi kuomba miezi sita iliyopita yamejibiwa.


Miezi sita iliyopita zilitokea nafasi za kazi Marekani za kwenda kufanya kazi kwenye kampuni ya tajiri wa kwanza wa dunia. Na wakatoa nafasi chache kwenye kila nchi wapate nafasi.


Ilikuwa ni Ndoto Yako ya muda mrefu kufanya kazi na kuishi nchini Marekani hivyo ulipoomba yale maombi ulitamani sana upate.Maombi yamejibiwa na umeshinda.


Huna pesa mfukoni unachotakiwa ni kujigharamia usafiri wa kwenda tu Marekani ukifika kule kila kitu kitakuwa safi.


Hivi unaweza kukaa tu nakusema sina hela, mfukoni nina elfu tano tu. Halafu usubiri tu bila kufanya Chochote?


Hapana hutafanya hivyo, utatafuta kila njia ili uweze kupata hiyo nauli ya kwenda Marekani.
Inawezekana na wewe una Ndoto kubwa lakini umekaa tu hufanyi chochote. Imebakia na sababu za Kila namna kwa nini huwezi.


Embu ichukulie Ndoto Yako kama kitu ambacho hakitajirudia tena. Unajua ukishaondoka hapa duniani kitu Pekee utakachoweza kufanya ni kujuta?
Embu jaribu kila njia kabla Hujasema Haiwezekani. Jaribu ili ukishindwa kuitimiza uwe na Ujasiri wa kusema nilijaribu, nilipambana mpaka mwisho.


Usikubali kukaa na kutoa sababu za kwanini huwezi badala yake angalia kile Kinachowezekana.Ndoto Yako Inawezekana, ukiamua itatimia. Usikubali kuishia njiani.


Nakutakia Kila la Kheri.

Ubarikiwe sana.

Rafiki Yako Jacob Mushi.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading