If you think you are beaten, you are;
If you think you dare not, you don’t.
If you’d like to win, but you think you can’t,
It is almost a cinch that you won’t.

If you think you’ll lose, you’re lost;
For out of the world we find
Success begins with a fellow’s will
It’s all in the state of mind.
-Stoic Later

Kila kitu huanza kwenye fikra, angalia mambo mengi unayopitia sasa hivi hayajatokea tu ghafla. Kuna namna ulishaanza kuyafikiri ndani yako.

Ulianza Kujiona huwezi, hufai, hustahili, utafeli na ndipo matokeo yakaanza Kuonekana nje.

Fikra ndio huongoza matendo yetu. Ukiwa na fikra za kushindwa hata ufanye kazi kwa bidii bado fikra za kushindwa ndio zitaleta matokeo.

Anza kubadili fikra zako kabla hata ya matendo. Hakuna mshindi aliewahi kutarajia kushindwa, fikra ndio hutupa Ujasiri au hofu. Fikra hutupa nguvu au unyonge.

Badili fikra zako ili Ubadili maisha yako. Sio Kazi Rahisi ni lazima ufanye maamuzi magumu, ujifuatilie kwa Karibu kile unachofikiri na uanze kukibadili taratibu.

Chukua Hatua Sasa, Ubadili Maisha Yako.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.
www.jacobmushi.com/coach

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading