467; #usiishienjiani leo: Unajisikiaje Unapofanya kazi Yako?

Ni muhimu sana uweze kujisikiliza na kutambua moyo wako unakwambia nini.
Moja ya vitu ambavyo tunakwama ni kushindwa kujisikiliza sisi wenyewe.

Unaweza kuwasilikiza wengine lakini huwezi kujisikiliza wewe unataka nini.

Mara nyingi ili. Uweze kujua kile unachokifanya kama ni kweli ni kusudi lako ni kuanza kusikiliza unajisikiaje unapofanya.
Kama unajisikiaje furaha fulani ambayo haielezeki ndani yako maana yake kile unachokifanya ndio umezaliwa kuja kufanya.

Kama kazi unayofanya wewe hujisikii hamasa yeyote hadi tarehe za mshahara zifike kuna tatizo.
Kama biashara yako unachojali zaidi ni faida unayopata kuliko watu wanavyosaidika maana yake hicho sio kitu chako.

Kabla ya vitu vyote cha kwanza kupimia kazi yako ni moyo wako na sio pesa. Ili mtu aweze kufanya kazi kwa bidii kwanza ni lazima aanze kuipenda kazi na kwa kuipenda kazi Ataweza kufanya kwa bidii kiasi ambacho kitaweza kumlipa.

Huwezi kupanga mipango mikubwa kwenye kitu ambacho hakileti furaha moyoni mwako. Siku zote mtu anaetaka Kudumu na wewe unamsikiliza anachokiongea. Ukiona mtu anasema tunasogeza sogeza tu maisha hapa ujue anachokifanya hakipendi.

Anza kupenda au acha katafute unachokipenda ufanye. Hapo utaweza kutengeneza matokeo makubwa sana.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.
www.jacobmushi.com/coach

This entry was posted in MAFANIKIO MAKUBWA on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *