Kuna mstari unasema “Kimtokacho mtu ndicho Kimjazacho” yaani kile unachoongea ndio kimejaa ndani yako. Ili uweze kubadilisha kinachotoka ndani yako anza kubadilisha unachoingiza ndani.


Ukiamka asubuhi unaanza kuingiza vitu gani kwenye ufahamu wako?Unaanza kusikiliza Habari na kutembelea mitandaoni ujue kiichotokea?
Anza kubadili unachoongea sasa kwa kubadilisha aina ya marafiki ulionao.Kama watu unaokaa nao mara zote huzungumzia umbea na Maisha ya wengine anza kuwakimbia.Kama wale unaoenda kubadilishana mawazo wanazungumzia zaidi mpira, mambo ambayo hayakujengi anza kuhama huko.


Jichanganye na watu ambao watakufanya ukue zaidi. Watabadilisha mazungumzo yako, uache Kuzungumzia matatizo uanze Kuzungumzia miradi mikubwa.


Huwezi kuanza ghafla Kuzungumzia biashara kama watu, vitabu, mitandao unayofuatilia kila siku haihusu biashara.


Anza kubadilisha kile unachozungumza kwasababu Unakua kile unachozungumza.


Nakutakia Kila la Kheri.

Ubarikiwe sana.

Rafiki Yako Jacob Mushi.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading