459; #USIISHIENJIANI LEO: Usiishi Kama Wanavyoishi Sasa.

jacobmushi
1 Min Read

“Dont live like rich people living currently, live the way they lived before being rich.”


Usiishi Kama matajiri wanavyoishi sasa, ishi kama walivyo kuwa wanaishi wakati wanautafuta utajiri.


Unaweza ukawa unafikiri kuishi kama matajiri ndio kuwa tajiri lakini ukawa unakosea. Wako watu huiga kila kitu kwenye maisha ya matajiri na kujikuta wamebeba mizigo mizito sana.


Mfano tajiri anapanda ndege binafsi, gari la gharama, hotel za kisasa na mengine mengi. Ukisema uige haya wakati bado hujawa tajiri pesa zako zote zitaishia huku na utaishia Kuonekana tajiri lakini sio uhalisia.


Vipo vitu vya kuiga na vyenye faida. Vitu hivi ni kama, Kuamka mapema, kusoma vitabu, kufanya mazoezi, kula vyakula bora, kuweka akiba, Upendo, na kadhalika.Haya yanafaa kuiga kwasababu ni tabia ambazo zinaleta utajiri na Maisha bora.


Kuna mtu aliwahi kusema usiige matumizi iga kutafuta. Ni kweli kwasababu kila mtu hutumia kulingana na kipato chake ukiiga unaweza kupotea.


Nakutakia Kila la Kheri.

Ubarikiwe sana.

Rafiki Yako Jacob Mushi.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading