“Gratitude is a duty which ought to be paid, but which none have a right to expect.” -Jean-Jacques Rousseau
Kushukuru ni wajibu wa kila mtu, Kulingana na wale waliokutendea mema lakini hakuna anaepaswa kutarajia shukrani kutoka kwa yeyote.
Haijalishi umewatendea mema wangapi kile kitendo cha kutaka wale uliowatendea wema wakuogope na kukutetemekea unakuwa unafanya makosa. Shukrani hailazimishwi.
Nimeshakutana na mtu anakusaidia kitu halafu baadae anakwambia unapaswa Kunishukuru sana kwasababu nisingekusaidia sijui ungekuwa wapi.
Hii ni hatari sana kwasababu hata Mungu anasema mtu wa aina hii Ameshapata thawabu yake hana tena chochote mbinguni.
Wewe usiwe mtu wa aina hii usipende kuwalazimisha watu wakushukuru. Kamwe usimwambie mtu hana shukrani, usiumie hata kidogo unapomtendea wema mwingine na asikuoneshe kujali.
Hilo sio jukumu lako, fanya kama Mungu anaenyesha mvua kwa wote hata kwa wale wanaomtukana usiku na mchana.
Kitu Pekee Ambacho hupaswi kusahau ni wewe kuwa mtu wa shukrani kwa kila jambo.
Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.
www.jacobmushi.com/coach