Mithali:26.27
Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.

Usikubali kuwa mtu anaewatendea wengine mabaya kwasababu huku ni kujitengenezea ubaya juu yako mwenyewe.
Unapomuumiza mtu humuumizi yeye peke yake kumbuka ana watu ambao wanamzunguka na wanampenda sana hivyo na wao husikia maumivu.

Kwa maana hiyo ni kwamba hata kama utafikiri umemkomesha mtu fulani kwa kumtendea ubaya ujue kuna vidonda umetengeneza kwa wengine ambao watataka kuja kudai haki baadae.

Maumivu yeyote unayoyasababisha kwa wengine ni kama shimo au jiwe ambalo unawasukumia wengine. Ipo siku na wewe shimo/jiwe hilo hilo litakuridia.

Leo tafakari kwa kina ni watu wangapi umewahi kuwaumiza na hujawaomba msamaha? Ni nani umewahi kumsingizia ili tu wewe uonekane bora?
Chukua Nafasi hii kumwomba msamaha kwasababu ipo siku hayo yatakurudia.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.
www.jacobmushi.com/coach

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading