447; USIISHIENJIANILEO: Sumbua Sumbua Watu Upate Haki Yako.

jacobmushi
2 Min Read

Nakumbuka mwaka 2016 nilifuatwa na watu mbalimbali wakiomba ushauri na Msaada wa Maisha na biashara. Mtu Anaweza kupiga simu akiwa na hamasa sana ukamwambia nipigie jioni tuongee vizuri, halafu asikutafute tena.

Jambo nililogundua ni kwamba Ukitaka kujua mtu amejitoa kiasi gani kwa ajili ya kile anachotaka msubirishe.

Kama ni kweli amejitoa na amedhamiria yeye mwenyewe ndio atakutafuta.

Kuna vitu vingine hutaweza kuvipewa tu mara moja pale ulipotaka. Hasa vile vyenye thamani kubwa.

Kama kweli Ndoto Yako ni ya muhimu kwako hutasubiria uletewe jambo mpaka mdomoni. Hutakata tamaa ukiambiwa hapana moja au hata kumi.

Ukubwa wa ndoto yako unapaswa uzidi ukubwa wa hapana za Wengine.
Ukimtafuta mtu akushauri halafu ukaogopa kumsumbua maana yake wewe Hujajua unachokitaka.

Kuna vingine hutapewa hivi hivi hadi Uonekane una nia ya dhati. Ulipokata tamaa tu yule mtu akasema kumbe hata ningemsaidia huenda ningekuwa napoteza muda wangu.

Endelea kusumbua hadi upewe haki yako.
Ione Ndoto Yako kama mtoto wako umpendae aliepo magereza na dhamana inasumbua. Hutakaa tu ukiambiwa Haiwezekani utajaribu kila kona, utampigia kila unaemjua, utasumbua watu wengi hadi upate msaada.
Fanya hivyo pia kwenye Ndoto Yako. Usiridhike na jibu la hapana endelea kusumbua.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading