Habari Rafiki, ninayofuraha kukujulisha kwamba Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi. Watakaofanya mambo makubwa leo hawana siku ya tofauti sana na wewe bali watafanya vitu vya tofauti kwenye siku hii.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“MIMI NI MSHINDI SIKU YA LEO, MALENGO YANGU YANAKWENDA KUTIMIA,
KILA NINACHOKIFANYA NINAFANYA KWA UBORA TOFAUTI NA JANA, SITAISHIA NJIANI HADI NDOTO YANGU ITIMIE, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Ukiwa juu ni rahisi sana kukosolewa.
Ukiwa juu hata yale mambo madogo madogo huonekana ni makubwa.

Ukiwa juu ni rahisi kutengeneza maadui usiowajua.
Ukiwa juu kila mtu anatamani kuwa karibu na wewe.

Inawezekana ukashangaa na kujiuliza kwamba mbona nilipokua sina kitu hakuna aliekuwa ananifuatilia?

Maisha ya mfalme Daudi yalibadilika baada ya kumuua Goliath. Alianza kupata marafiki hadi watoto wa mfalme Saul (wakati huo yeye hakuwa mfalme bado).
Alianza pia Kutengeneza maadui na Marafiki wengi.

Ninakutia moyo usonge mbele ufikie Ndoto Yako kubwa lakini jiandae kwa haya mambo mbalimbali yatakayojitokeza.

Kumbuka tu kwamba Daudi alipokuwa anampokonya Simba Mwana Kondoo hakuna aliejua wala kuyafuatilia maisha yake.

Lakini baada ya kumuua Goliath kila kitu kilibadilika. Baada ya wewe kushinda jaribu ulilonalo mambo mengi yatabadilika.

Utahamishwa viwango vingine, ukiwa viwango vingine tarajia changamoto zingine, majaribu mengine, maadui wengine.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI
Ubarikiwe sana,
Rafiki Yako, Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading