Habari Rafiki, ninayofuraha kukujulisha kwamba Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi. Watakaofanya mambo makubwa leo hawana siku ya tofauti sana na wewe bali watafanya vitu vya tofauti kwenye siku hii.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“MIMI NI MSHINDI SIKU YA LEO, MALENGO YANGU YANAKWENDA KUTIMIA,
KILA NINACHOKIFANYA NINAFANYA KWA UBORA TOFAUTI NA JANA, SITAISHIA NJIANI HADI NDOTO YANGU ITIMIE, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Musa baada ya Kumaliza kusudi lililompelekea kwenda kulelewa kwa farao alianza kuzoea yale maisha.
Wakati huo huo Mungu alikuwa ameshaandaa mpango mwingine.

Na ule mpango ili utimie ilipaswa kutokee kutokuelewana. Ndipo Musa akakutana na Mmisri na Mwebrania wanapigana.

Kwa kumuua Mmisri ikawa ndio sababu ya yeye kuondoka Misri kwa ajili ya kusudi la pili.

Wakati mwingine kuna mambo yanatokea kwenye maisha kwa lengo la kukuondoa sehemu moja uende nyingine.

Huenda ulifukuzwa kazi kwasababu Mungu amekupangia kusudi lingine kubwa zaidi. Huenda umepata hasara kwenye biashara kwasababu unatakiwa uache hiyo biashara ukaanze nyingine au ukafanye kitu kingine kabisa.

Ukiendelea kung’ang’ania sehemu ambayo Mungu anato uondoke Kamwe huwezi kufanikiwa hapo.
Fuata kule Mungu anataka uende.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI
Ubarikiwe sana,
Rafiki Yako, Jacob Mushi
https://jacobmushi.com/kocha/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading