Moja wapo ya vitu vinavyofanya watu wakose furaha katika safari hii ya maisha na mafanikio ni kujifanananisha na wengine. Unakuta mtu anajiona yeye si kitu pale anapokutana na mtu mwenye vitu zaidi ya yeye alivyo navyo.

Mfano mzuri ni kipindi hiki watu wengi wana simu aina ya smartphone. Mtu anajihisi ili aonekane wa maana itabidi awe na simu ya ghali zaidi kuliko wengine. Mtu anajibana na kama anategemea mshahara atajibana kweli ili anunue simu ya ghali. Kiukweli sio vibaya kama unanunua kwa ajili ya matumizi fulani ila kama unanunua ili watu wakuone na wewe unayo ya ghali huko ni kujitesa tu fanya kile kitu kilichopo ndani ya uwezo wako au kutokana na matumizi yako ynahitaji nini. Ukifanya mambo kuwaridhisha watu kamwe hutakaa uwe na furaha utakua unateseka moyoni nyumbani unashindwa kula vizuri ili watu wakuone una simu nzuri na ya gharama.

Unakuta mtu kaona labda watu aliosoma nao tayari wamenunua magari. Na yeye bado anatembea kwa miguu. Basi atakwenda na yeye kukopa ili anunue gari ili asipitwe na yeye afanane nao. Kiukweli utaonenakana na wewe upo kwenye level nzuri utasifiwa ila ukishindwa kulipa mkopo hakuna ambaye atajua.  Ukilala njaa ili upeleke marejesho ni weww mwenyewe sio wale wanaokusifia mtaani na kazini kwako.

Unakuta mtu anajua kabisa kutokana na kipato changu kwa sasa siwezi kuishi kwenye nyumba ya gharama fulani labda tuseme kwenye self container.  Lakini kutokana na watu anaowajua anatembea nao kila siku wanaishi kwenye nyumba nzuri apartments za gharama na yeye anataka kufanana nao bila kuangalia kipato chake bado hakijakua.  Ndio utafanana nao lakini mateso yatakua juu yako mshahara utaisha kabla ya mwezi kufika nusu utaishia kulalamika mshahara hautoshi kumbe ni wewe mwenyewe umeufanya usitoshe.

Angalia vile vitu vinavyoendana na kipato unachoingiza huku ukitafuta namna ya kukuza Kipato ili uweze kutoka sehemu moja kwenda nyingine usiangalie wengine wana nini na wewe huna nini usijilinganishe na wengine fuata malengo yako.  Fuata vipaumbele vyako. Kila jambo linaanza kwa hatua hata huko utafikia lakini usijifikishe utajipa madeni na mizigo ambayo haikustahili.

Mtu mmoja akaniambia kuna rafiki yake alikua na million 50 bank akamuona mwenzake mtaani kanunua gari ya million 40.  Na yeye kwa kutaka aonekane ni mwanaume akaenda bank akachukua pesa akaenda kununua gari ya million 40 ili tu afanane na mwenzake. Mwenzake ana biashara kubwa zinazo mwingizia kipato na anaweza kulihudumia gari lake. Yeye amebakiwa na million 10 bank inabidi sasa akazitoe ili aweze kuweka mafuta na kufanyia gari service.  Jiulize baada ya miezi sita huyu jamaa alieiga atakua kwenye hali gani ya maisha na gari lake la million 40.

Kua na malengo ya maisha. Fanya kazi kwa bidii na maarifa. Fuata vipaumbele vyako mafanikio ni lazima. Usikate tamaa.

©Jacob Mushi 2016
Niandikie 0654726668 Whatsapp E-mail jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading