USIKATE TAMAA

“We are all dreamers creating the next world, the next beautiful world for ourselves and for our children.” Yoko Ono

Sisi wote tuna ndoto za kutengeneza dunia ijao, dunia ijao bora sana kwetu sisis na kwa watoto wetu. Usiache kua na ndoto kubwa na kuifanyia kazi. Haya yoote uyaona mazuri yaliyopo duniani sasa hivi kuna watu walikua na ndoto hizo miaka ya nyuma na wakazifanyia kazi ndio maana tunaona mabadiliko makubwa. Wewe pia unayo nafasi ya kufanya dunia iwe mahali bora Zaidi pa kuishi wengine kwa kutimiza ndoto yako.
Ndoto yako ni ya maana sana, haiko bure kwako ni kwa ajili ya kuifanya dunia iwe bora. Embu jiulize aliekua na ndoto ya kutengeneza laptop angekata tamaa ingekuaje? Labda tusingekua na kitu hiki. Na wewe ni nafasi yako kufanya mabadiliko kutokana na kile unachokiota leo.
Changamoto zipo na utakutana nazo hakuna kitu utafanya katika dunia ya sasa kifikie mafanikio makubwa kirahisi. Lazima upitie changamoto kwasababu njia unayoiendea hujawahi kuipita. Ndoto ulizonazo hujawahi zifikia. Kuna tofauti kubwa sana ya changamoto atakazopitia Mengi anapoanza biashara inayofanana na ya kwako kabisa inawezekana asipitie changamoto yeyote kwasababu yeye alishapita huko unakopita wewe.
Usikate tamaa ongeza maarifa yako juu ya kile unachokifanya hakikisha unafikia maono yako. Inawezekana.
Jacob Mushi
0654726668
Siri 7 za Kua Hai Leo.
This entry was posted in USIISHIE NJIANI on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

2 thoughts on “USIKATE TAMAA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *