Unawajibika kwa kila hali inayoendelea kwenye Maisha yako. Lolote linalotokea kwenye Maisha yako wewe unahusika kwa asilimia mia moja kabla hujatupa lawama kwa mwingine yeyote.

Unaweza kuamua uwe na furaha au uwe na huzuni.
Unaweza kuamua kuwapenda wengine, kutenda wema kwa wengine au kufanya kinyume chake.

Kuna jambo moja pekee ambalo unaweza kufanya ili uweze kuishi Maisha yasiyo na maumivu ya ndani. Ni hatari sana kama utakuwa unaishi huku ndani yako unaumizwa na mambo Fulani Fulani yanayoendelea Maishani mwako au yaliyokwisha kupita.
Unaweza kutengeneza Maisha mazuri kwa kuamua kutoweka moyoni mwako jambo lolote lile ambalo linakufanya ukose Amani, furaha na hata kushindwa kufikiri vizuri. jambo lolote ambalo linakuja kukuvuruga ili ushindwe kusonga mbele usikubali likae moyoni mwako.

Usikubali kuweka chuki ya aina yeyote ile ndani ya moyo wako.

Usiweke kinyongo na mtu bila kujali amekufanyia kitu gani.

Usijenge visasi kwa namna yeyote ile.

Usikubali jambo ambalo huwezi kulidhiti liutese moyo wako hasa kama hauna uweze wa kudhibiti kwa 100%.

Maisha yako unaweza kuamua namna ya kuishi wewe mwenyewe usikubali kuishi kama binadamu wengine wanavyotaka.

Miliki Maisha yako kwa 100%, yajue majukumu yako. Hakikisha una furaha na Amani kila wakati ndio maana ya Maisha bila kujali unapitia ugumu wa aina gani. Usikubali ugumu wa Maisha uwe sababu ya wewe kukosa Amani na furaha.

Ni Mimi Rafiki Yako Jacob Mushi…


Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,
Simu: 0654 726 668,
Twitter: jacobmushitz
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading