Ni kweli hakuna kuchelewa katika mafanikio yaani hata kama una miaka 60 sasa hivi bado unaweza kuchukua hatua na kuitimiza ndoto yako. Wapo pia watu wanasema kama umepangiwa kufanikiwa utafanikiwa tu, kama umepangiwa kuwa maskini utakuwa masikini hata upambane vipi.

Hayo ni aina ya mawazo ambayo unaweza kuwa nayo na yakawa sababu ya wewe kuendelea kuchelewa kuifikia ndoto yako. Ukweli ni kwamba hakuna ajuae ataishi hadi lini. Hakuna ajuae kesho itakuaje ila kila mmoja anaweka mipango mbalimbali ya Maisha yake.

Kwanza ondokana na fikra mgando kwamba kama umepangiwa itatokea tu. Hakuna kitu kama hicho kwenye dunia hii wenye nguvu, wenye maarifa, wanaochukua hatua bila ya kusita ndio hufikia mafanikio makubwa. Mungu hakukuumba na kukupa wewe akili ya bure. Kama wewe utaishia kuitumia akili yako kufanya vitu vya kawaida ni kwa uzembe wako kuwa masikini.

Usiseme kwamba ipo siku itatimia ndoto yako halafu hakuna chochote unachokifanya. Kama ndoto yako ni kuwa mwimbaji mkubwa anza kuimba sasa acha kusubiri. Acha kusubiri hadi ujisikie vizuri au mambo yawe mazuri ndipo uanze kuimba. Acha kusubiri hadi upate pesa ya kuvaa vizuri ndipo uanze kuimba.

Una kipaji cha kuandika anza kuandika hata kwenye daftari usisubiri hadi upate Compyuta. Hakuna mtu atakae ona kile kilichopo ndani yako kama wewe utaendelea kusema ipo siku mambo yatakuwa sawa na hufanyi chochote cha maana.

Usisubiri hadi ujisikie vizuri wakati mwingine unapaswa kujilazimisha kufanya kile ambacho unapaswa kufanya hata kama unajisikia kuchoka. Ndoto haiwezi kuwa kweli kama hujaweka juhudi zozote. Hakuna kitakachotokea bila ya wewe kuweka juhudi za kutosha.

Naendelea kukmwambia acha kusubiri mambo yakae sawa, acha kusubiri pesa uliyoahidiwa ndio uanze biashara, acha kusubiri chochote anza na kile ambacho kinawezekana sasa hivi. Ukiendelea kusubiri utasubiri sana na hakuna kitakachotokea.

Napenda pia kukukumbusha kwamba hakuna mtu mwingine anayafikiria Maisha yako kuliko wewe mwenyewe, sio serikali, sio wazazi wako, sio ndugu yako yeyote yule. Kila mmoja ana mambo yake anayawaza sana. Acha kupoteza muda kusubiria jambo ambalo wewe hujaweka juhudi zozote katika kulifanya litokee.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

2 Responses

  1. Mungu akubariki sana kaka jumbe zako hizi zinanibariki sana na kuubadilisha Ufahamu wangu kila nisomapo.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading