USITAZAME NYUMA

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Ulikotokea hakuna maana kubwa sana kama unapoelekea, haijalishi una historia ya aina gani bado unaweza kuibadilisha leo.

Acha kurudi nyuma na kuangalia kule uliwahi kushindwa, maisha yanaweza kubadilika kwa vyovyote vile unavyotaka.

Unaweza kutengeneza tena leo haijalishi wiki iliyopita ulikosea kiasi gani kama bado upo hai una nafasi ya kubadilisha  baadae yako.

Inawezekana watu wanakusema na kukudharau kwa matendo yako au makosa uliyowahi kuyafanya lakini wewe usiwaangalie muangalie Mungu aliesema atakusamehe dhambi zako.

Inawezekana watu wanakuhukumu kutokana na historia yako hao ni wanadamu ukiwaangalia utakua unakosea sana muangalie Mungu msamehe dhambi aliekufia msalabani, aliesema atakusamehe.

Mungu yeye haangalii mwanzo wako haangalii umeanzaje anaangalia umemalizaje kuwepo kwako hai ni sababu maalumu ya kubadilisha maisha yako.

Nakutakiwa Baraka na mafanikio katika kila unachokwenda kukigusa ukafanikiwe, mafanikio yako ndani yako, una nguvu inayokupeleka kwenye mafanikio makubwa.

Usikate tamaa haijalishi unapitia hali ya namna gani kwa sasa hautabakia hivyo milele, hali uliyonayo sasa ni ya muda tu usiiangalie.

Dunia inakwenda kuona mabadiliko makubwa kutoka kwako, inakwenda kuona vile vitu Mungu alivyoweka ndani yako.

Inuka ukaangaze kwa maana nuru ya Bwana imekujilia uwezo wa Kimungu upo ndani yako. Unaweza kufikia chochote kile unachokitaka.


Isaiah 60King James Version (KJV)
60 Arise, shine; for thy light is come, and the glory of the Lord is risen upon thee.
2 For, behold, the darkness shall cover the earth, and gross darkness the people: but the Lord shall arise upon thee, and his glory shall be seen upon thee.
And the Gentiles shall come to thy light, and kings to the brightness of thy rising.
 Maisha yako yanakwenda kubadilika usitazame nyuma usiwatazame wanadamu, tazama mbele mtazame Mungu, umelibeba kusudi lake.
Karibu sana.
#Jacob_Mushi
#0654726668

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading