Usiwe na Tabia za Maji.

By | February 2, 2018

Maji hayana umbo wala rangi, ukiyaweka kwenye chombo chochote kile yatachukua rangi ya chombo na umbo la chombo.

Ukiyamwaga chini yatachukua vilevile rangi ya pale uliyoyamwaga.

Maji siku zote hayana utaratibu yanafuata mkondo uliopo mbele na kuanza kutiririka. Pia yasipowekewa utaratibu mzuri huleta uharibifu mkubwa.

Maji hayawezi kupanda mlima siku zote yanakimbilia mabondeni, ukitaka kuyapandisha kwenye mlima lazima utumie nguvu ya ziada.

Wewe Rafiki yangu usikubali kuwa kama maji kwasababu maji hayaeleweki. Popote ukiyaweka yanakaa, ukiyachanganya na chochote yanakubali.

Watu wenye tabia za maji hawadumu kabisa kwenye mafanikio. Wakifanya vitu mara nyingi wanaishia njiani.

Watu hawa ni rahisi sana kubadilika hasa pale wanapokutana na vitu vipya. Sio watu wa kuwaamini na kuwaachia vitu bila ya uangalizi.

Wakizidiwa wanaweza kufanya uharibifu mkubwa kwao na kwa wengine.

Watu wenye tabia za maji mara nyingi hawawezi kusimama wenyewe lazima wabebwe na wengine au wasimamie vitu vya wengine.

Ukitaka kuwa mtu mkuu lazima ukubali kubadilika na kuachana na tabia za maji.

Kuwa na msimamo,

Eleweka rangi yako ni ipi.

Eleweka tabia zako ni zipi.

Jifunze kusimama mwenyewe.

Jitahidi watu wakuamini.

Usipende kuhurumiwa hurumiwa.

Simama na tekeleza majukumu yako mwenyewe.

Rafiki maji ni uhai lakini siku ukiwa katikati ya bahari unazama ndio utajua huo msemo wa maji ni uhai haukuwa umekamilika vizuri.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Simu: 0654 726 668,

Twitter: jacobmushitz

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page  

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

 

One thought on “Usiwe na Tabia za Maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *