USIYAFANYE MAISHA YAKO KUWA MAGUMU (Sehemu ya 3)

jacobmushi
By jacobmushi
4 Min Read

Kokosa Vipaumbele.

Hakuna Maisha ya hovyo na magumu hapa duniani kama Maisha yasiyo na vipaumbele. Rafiki yangu lazima ujue una mambo gani unatakiwa kufanya na hayo mambo yasiweze kuingiliwa na ratiba nyingine yeyote isiyo ya umuhimu.

Kuna watu wanaishi Maisha ya ajabu kweli yaani unakaa unangojea jambo litokee ndio uchukue Hatua. Unasubiri wanaokudai watakuaibisha ndipo upambane kutafuta hela. Unangojea yatokee majanga kwenye Maisha yako ndipo uanze kujua nini cha kufanya.

Kama mwanadamu unaejitambua unapaswa kuwa na angalau mambo makuu 3 hadi matano au tunasema vipaumbele vikuu ambavyo unavipigania hapa duniani hadi mwisho wako.

Jambo la kwanza linapaswa kuwa kusudi la wewe kuwepo hapa duniani. Na ndani ya kusudi ndio kuna maono na malengo ya hilo kusudi. Ili tuseme kusudi lako ndio kipaumbele chako kikuu lazima angalau iwe kila siku unafanya jambo linalohusiana na kusudi lako.

Lazima uweke kipaumbele cha kuwa na afya bora bila afya huwezi kufanya chochote kwa ufanisi. Kama afya yako ni kipaumbele basi hakikisha kila siku unakula vizuri na kufanya mazoezi.

Lazima uwe na kipaumbele cha familia kama una watoto na mwenzi wako basi na wao wawepo katika vipaumbele vyako vitatu vya kwanza. Lazima uhakikishe kila siku itokayo kwa Mungu umewaweka kwenye ratiba yako. Uwe umefanya jambo kwa ajili yao, ikiwa ni pamoja na kuongea nao.

Unaweza kuendelea kuongeza vipaumbele vingine biashara, kazi, na sehemu zile ambazo zinakufanya wewe kuwa bora Zaidi.

Ni rahisi sana kumfahamu mtu jinsi alivyo kwa kutazama vipaumbele vyake.

Ni rahisi sana kujua mahali mtu anakwenda kwa kutazama vipaumbele vyake.

Ugumu wa maisha utaongezeka kama utaendelea kuvipa kipaumbele vitu ambavyo haviongezi thamani kwako. Utakuwa unapoteza muda na kufanya Maisha kuwa magumu kama utaendelea kufanya vitu ambavyo matokeo yake ni madogo na hayana mchango mkubwa kwenye maendeleo yako.

Tengeneza vipaumbele, jua ni kipi cha kufanya sasa, kipi cha baadae. Vitu gani utasema hapana na vitu gani utasema ndio.

Watu gani utawakaribisha kwenye Maisha yako na watu gani huwezi kuwapa nafasi hata kidogo. Aina gani ya maarifa unahitaji kwa wingi Zaidi. Aina gani ya ujuzi unapaswa kujifunza ili uwe bora Zaidi.

Usiache kuwa na vipaumbele kwenye Maisha yako. Maisha yanakuwa magumu kwasababu tunavipa nafasi Zaidi vitu na watu wasio na umuhimu kabisa kwenye Maisha yetu. Kama ukiweza kujua ni kipi cha muhimu kufanyika kwa sasa na kipi ni cha baadae lazima utaona mabadiliko na maendeleo kwenye Maisha yako.

KUJIFUNZA HAYA ZAIDI:

Jiunge na kundi letu la WhatsApp la Usiishie Njiani Academy. Kuwepo kwenye kundi hili unapaswa ununue vitabu 3 tu ambavyo vinatolewa na Usiishie Njiani Academy.

Vitabu hivyo ni:

MAFANIKIO KWENYE BIASHARA (10,000)

SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO (10,000)

MBINU 101 ZA MAFANIKIO (10,000)

USIISHIE NJIANI TIMIZA NDOTO YAKO (5,000)

UMUHIMU WA MAONO (3,000)

Vitabu vyote vinapatikana kwa njia ya mtandao yaani softcopy unalipia kisha unatumiwa kwenye email yako. Namba za malipo ni 0755192418 au 0654726668 jina ni Jacob Moshi

Karibu sana Rafiki.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading