Maneno yako yanajenga vitu kwenye maisha yako, hata kama hutaona matokeo yake kwa muda huu ipo siku yataonekana hata ikiwa umeshasahau. Ni vyema sana kujitazama sana kile uanchokiongea kinaweza kuleta matokeo gani kwenye maisha yako na kwa wengine. Sio kila neno ni la kutamka, sio kila jambo ni la kuchangia unaweza kujikuta unajichimbia shimo mwenyewe.
Sina maana ya kwamba ukae kimya kila mahali bali ni uweze kuwa na hekima ya kutambua kwamba wakati huu ndio wakati sahihi wa kusema jambo hili. Unaweza kutengeneza matatizo badala ya kutatua tatizo moja kwa kukosea kuongea.
Kile unachokisema kitakuletea matokeo katika maisha yako.
Kama muda mwingi unatumia kuzungumza umbeya utakula matunda ya umbeya.
Muda wako mwingi na story zako ni za kijinga Zaidi utakula matunda ya ujinga unaoongea.
Umefikia mafanikio makubwa unaanza kuonyesha dharau kwa wanaokufuatilia utakula matunda ya dharau.
Ukizungumza maneno ya kujenga wengine ipo siku utakuja kula matunda yake.
Yale unayoayaandika kwenye mitandao ipo siku utakuja kuona matunda yake.
Picha zisizoeleweka unazopost kwenye mitandao ya kijamii ipo siku utakula matunda yake.
Endelea unavyotumia mdomo wako vibaya ipo siku utakuletea matokeo.
Neno la Mungu linasema kila neno ulilolinena linahesabiwa. Hakikisha unachokizungumza kina maana kwako na kwa wengine.
Madhara ya kuongea ongea hovyo vitu visivyo na maana ipo siku utakuja kuona matokeo yake.
Neno la Mungu linasema maneno ya kinywa changu yapate kibali mbele zako yaani mbele za Mungu. Kama unayoyaongea hayapati kibali mbele za Mungu bora uyaache mara moja.
Hakikisha unalolisema linamjenga mtu na kumpeleka sehemu nyingine bora Zaidi ya ile aliyokua.
Kabla hujaongea lolote embu jaribu kulitazama ingekua ni wewe unaambiwa hivyo ungejisikia furaha? Ungetabasamu?
Ubarikiwe sana,
Rafiki Yako, Jacob Mushi