Mara nyingi tunapenda Zaidi kufanya yale ambayo yanawezekana kwenye uwezo wetu wa akili. Sio vibaya lakini unakuwa hakuna cha tofauti ambacho utakipata.
Watu wote ambao wameweza kugundua mambo makubwa na yakaleta mapinduzi kwenye dunia na kwenye Maisha yao walijaribu yale ambayo yalionekana kama hayawezekani kabisa.
Vile vyote ambavyo vinawezekana vinakufanya wewe uwe sawa na wengine wote. Wewe kama mjasiarimali unapaswa kujua kwamba kama unataka kuleta mabadiliko makubwa kwenye unachokifanya kubali kujaribu yale ambayo yanaonekana hayawezekanagi.
Kuna mambo ambayo wamesema kwamba watu wengi wamejaribu wakashindwa basi hiyo ndio sehemu yako ya kutokea. Ukiweza kufikiri vyema na Zaidi ya wengine utagundua namna ya kutatua kile kilichoshindikana.
Unapochukua Hatua ndogo ndogo kwenye vile vitu vinavyoonekana ni vigumu unakuwa unaijenga akili yako na kuifanya iamini juu ya uwezekano.
Kama Mjasiriamali ni lazima ujue kwamba wewe kukua ni lazima, kile ulichokianzisha kisiishie kuwa kama wengine ambao walishafanyaga. Hili litawezekana pale ambapo utaamua kujaribu vile vitu ambavyo vinaonekana kama hakuna uwezekano.
Lazima ukubali kuwa na nguvu ya uthubutu wa kuchukua Hatua kwenye vile vitu ambavyo vinaonekana haiviwezekani.
Lazima uwe na Imani ili uweze kupata nguvu ya kuchukua Hatua bila ya kusita sita. Imani yako ndio inakuamulia nguvu ya kuchukua Hatua.
Usikubali ukomo aliojiwekea mtu mwingine ukawa ni ukomo wako wewe. Amini inawezekana na chukua Hatua.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Author | Trainer | Entrepreneur
Simu: 0654 726 668 |0755192418,
Twitter: @jacobmushitz
Instagram: @jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com