VITU 5 UNAVYOPASWA KUVIFAHAMU ILI UWEZE KWENDA NA KASI YA MABADILIKO-9/11/2018

jacobmushi
4 Min Read

Tupo kwenye dunia ambayo kila kukicha kunakuwa na mabadiliko mapya katika sehemu mbalimbali hasa za kiteknolojia. Kama mwanadamu ukishindwa kwenda na kasi hii kuna mambo mengi utajikuta unashindwa kufanya au unalipa gharama kubwa sana ili tu yafanyike.

Kuna vitu vingi ambavyo ungevijua vingeweza kuwa rahisi sana kwako kugundua fursa mbalimbali ambazo zingekuingizia kipato. Kwasababu hujafahamu nah una ujuzi wowote unajikuta umekaa chini na kuendelea kulalamika.

Mtandao wa Internet.

Ni kweli unaweza kufikiri unajua kutumia intaneti lakini kumbe vile unavyovijua ni vichache sana au havina umuhimu sana. Mtandao wa intanet unapaswa kuufahamu tu namna ambayo unafanya kazi ili uweze kufanya vitu mbalimbali. Inawezekana wewe unajua kuingia Google na kutafuta kitu pekee lakini hujawahi kufikiri kwamba na wewe unaweza kuweka vitu vyako mtandaoni ili watu wakiingia Google kutafuta wavione.

Barua Pepe (Email Adress)

Unaweza Kushangaa labda hakuna ambaye hajui kutumia barua pepe? Ndio wapo wengi sana wana barua pepe kwenye simu zao za smartphone lakini hawajui namna ya kuzitumia. Kwa karne ya sasa kama hujui kutumia email utakuwa unakosa vitu vingi sana. Ukitaka kuomba kazi siku hizi unaambiwa utume maombi kwa barua pepe. Ukitaka kufungua application mbalimbali zinataka uwe na barua pepe.

Lazima ujifunze kutunza na kuikumbuka barua pepe yako. Kuna vitu vya muhimu kama nakala za vyeti vyako au barua mbalimbali unaweza kuzihifadhi kwenye barua pepe. Ukipata dharura mahali unazihitaji hizo nakala inakuwa rahisi kwako wewe kwenda kuchapa.

Kuna mafunzo na elimu nyingi zinatolewa na kwa njia ya barua pepe. Wewe kama hadi sasa hujui kutumia au hutumii mara kwa mara inakupasa uanze kujifunza kutumia.

Compyuta (Computer)

Ni kweli comptyuta pia ni muhimu sana, unapaswa kuifahamu japo kwa uchache. Badala ya kutumia kuangalia movie au kufanyia kazi ya darasani tu hasa kwa wanachuo embu jaribu kuwaza kujifunza vityu vingine ambavyo vingeweza kukunufaisha.

Unaweza kuwa na smartphone lakini kama hujui kutumia compyuta kwenye karne hii kuna kazi nyingi unaweza kuzikosa. Huu ni ujuzi unapaswa kila mmoja awe nao.

Blogu (Blog)

Ndio unaweza kusema sasa blog ya nini? Unapaswa kuijua blog na unapaswa kuwa na blog yako. Kwenye blog unaweza kuandika kitu chochote ambacho unataka wengine wajue kuhusu wewe. Unaweza kuamua kuandika yale ambayo unapitia na kujifunza kila siku kwenye Maisha yako ili wengine wajifunze kwako.

Kama wewe ni kijana wa karne hii na hujui kutumia blog unachelewa sana. Embutafuta namna ujifunze na uwe na blog yako.

Utumiaji wa Mitandao ya Kijamii.

Hii ndio inaonekana ni ya muhimu sana kuliko vyote lakini ukweli ni kwamba kama hujui kutumia email, kama hujui kutumia mtandao wa intanet hii mitandao ya kijamii itakushinda. Unaweza kuibiwa, unaweza kupoteza account zako kwasababu ulishindwa kufahamu mambo machache tu.

Mitandao ya kijamii watu wengi hawajui kuitumia. Kwa kifupi jifunze namna inavyofanya kazi na angalia ni namna gani unaweza kufaidika nayo. Usiishie kuingia huko na kuangalia Maisha ya wengine na kufuatilia habari. Embu jaribu kuwaza ni namna gani unaweza kuitumia kuwasaidia wengine na wewe uwe umefaidika.

Vitu vitu vingi sana unaweza kufanya kwa kutumia mitandao hii na ukaweza kuwafikia watu wengi na ukafaidika. Umemaliza chuo huna kazi unajua inawezekana wewe kutumia elimu uliyotoka nayo chou kutengeneza kipato kwa kutumia mitandao hii?

Una ujuzi Fulani kwenye Maisha, ujuzi huo umekaa nao tu na unasema hakuna fursa unajua unaweza kuutumia ujuzi huo ukatengeneza kipato? Swali linakuja je umejifunza? Umeweza kuona fursa? Una mtu wa kukuongoza?

Karibu sana Rafiki yangu, kwa ushauri kuhusu masuala ya mtandao wa intanet unaweza kuwasiliana na mimi. Nimeanza kutumia intanet tangu mwaka 2008 hivyo ninaweza kukusaidia popote unapokwama.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading