Kuna vitu saba vya muhimu ambavyo ni lazima uvijue ili uweze kuanza kusonga mbele kimaisha.  Ukiweza kuvichukua na kuingiza kwenye maisha yako utaona matokeo yake.

1.ELIMU
Kitu cha kwanza kwenye vitu FISA ni Elimu.  Tunapozungumzia elimu hatumaanisha uwe na elimu ya chuo kikuu au ujue kila kitu hapa unatakiwa uwe na ufahamu wa kutosha juu ya kile unachokifanya. Kama ni kilimo kifahamu vizuri kilimo. Pata taarifa za kutosha kwenye kile unachokifanya.  Ukitaka kupata mafanikio zaidi unatakiwa ujifunze zaidi.

2. UJUZI
Kitu cha pili ni UJUZI. Utapata chochote unachokita ukiwa tu na ujuzi wa kutosha juu ya kile unachokifanya. Matokeo bora unayoyapata kwenye kazi yako ndio yatasababisha wewe usonge mbele. Unaongeza ujuzi kwa kupitia kujifunza na uzoefu wa kufanya vile unavyojifunza unapofanya vitu vidogo vidogo vinaongeza matokeo bora zaidi.

3. WATU UNAOWAFAHAMU
 Kitu cha tatu unachotakiwa kukifahamu na kukiongeza ni watu ongeza watu wapya kila ili uweze kupata matokeo bora mfano wewe unafanya kilimo cha biashara lazima ufahamu watu wengi zaidi kila siku wanaolima kama wewe, wateja, na watu ambao unaweza kupata maarifa zaidi kutoka kwao. Kila mtu unaekutana nae anaweza kua sababu ya Kukuza Biashara yako anaweza kua fursa mpya katika kile unachokifanya. Wafahamu watu wengi zaidi upate mafanikio zaidi.  Na usiishie tu kuwafahamu lakink uwe na mahusiano bora mahusiano bora ndio yatafungua milango ya fursa.

4. PESA
Kitu kingine ni pesa unahitaji pesa ili uweze kupata uhuru na uwezo wa kuchukua fursa mbalimbali zinapotokea. Kama umefilisika na una madeni ni ngumu Sana kupata milango ya fursa ikifunguka mbele yako. Kama huna uchaguzi huna uhuru.

5. TABIA YA UBORA KWENYE KAZI.
kitu kingine cha muhimu ni tabia ya ubora kwenye kazi. Kila unachofanya hakikisha unakifanya katika ubora wa hali ya juu.   Na ubora katika ufanyaji wa kazi unaletwa na kufikiri kabla hujafanya lazima ujue ni matokeo gani unayoyataka kwenye kazi ile unayoifanya.

6. MTAZAMO CHANYA
Ili uweze kutimiza malengo yako lazima uwe na mtazamo chanya.  Mtazamo chanya haujengwi kwa siku moja ni kitu ambacho kinafanyika kila siku mpaka kinakua kimejijenga kwenye maisha yako. Mtazamo chanya utakusaidia sana katika maamuzi unayoyafanya kila siku kwenye kazi/biashara au hata maisha yako ya kawaida.

6. UVUMBUZI
Kitu kingine ni uvumbuzi ili uweze kusonga mbele lazima uwe mvumbuzi usifanye mambo kwa njia zile zile za kawaida vumbua njia mpya kila siku za kuboresha biashara au kazi hata mahusiano yako.

7. TABIA
Tabia ni sababu ya muhimu sana katika maendeleo yako ya kila siku na ili uweze kupata mafanikio makubwa lazima uwe nidhamu binafsi, uaminifu kwenye kila jambo watu wanapokuamini wanaweza kukupa chochote kile mikononi mwako. Vitu ulivyoahidi kuvifanya vifanye maana vitaongeza watu kukuamini.

Asante sana kwa kusoma makala hii naimani umejifunza kitu.
Asante sana na Karibu
©Jacob Mushi 2016 Tuandikie 0654726668 E-mail jacob@jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading