Habari rafiki, kwenye maisha ya sasa ili uweze kuishi maisha yale ambayo unayotaka kwa zaidi ya 50% lazima uwe na njia mbalimbali za kukuingizia kipato. Usikubali kutegemea njia moja ya kukuingizia kipato. Hata kama sasa unategemea njia moja anza mpango wa kutengeneza njia nyingine kwa ajili ya vipato.

Biashara nyingi kubwa zinaweza kujiendesha zenyewe na kudumu muda mrefu kwasababu ya mifumo ambayo imejengwa na wamiliki wa biashara hizo. Ni muhimu unapojenga biashara angalia kwenye mifumo yako ili uweze kutengeneza kitu imara na kitakachodumu. Nimezungumza haya kwa kina kwenye Kitabu changu cha BIASHARA 101 utakipata uweze kujifunza zaidi.

Matajiri wote duniani wa mifumo.

•  Matajiri wote duniani wametengeneza mifumo inayowaingizia pesa kila siku bila ya wao kuweka muda wao.

•  Biashara unayoianza leo inatakiwa baada ya muda iweze kujiendesha yenyewe.

•  Unapokua na mifumo mingi inayokutengenezea pesa na pesa zako zinakua nyingi.

•  Kamwe usitegemee mfumo mmoja wa kukutengenezea pesa mfumo mmoja unapopata shida unakua upo salama kwani kuna mingine imesimama.

•  Hakikisha  mifumo uliyonayo inakua kila siku yaani faida inaongezeka.

•  Tuseme una mifumo 10 ambayo inakuletea Tsh 10,000 kila siku ni sawa na 10,000×10=100,000/= wewe utakua tofauti kabisa na mtu mwenye mfumo mmoja. Kipato chako kwa mwezi kitakua ni 3,000,000/=

•  Pia unaweza ukawa na mifumo michache inayotengeneza kipato kikubwa mfano una mifumo mitatu inayokuletea Tsh. 100,000/= kwa siku ni sawa na Tsh. 300,000/=

•  Kwa hiyo haijalishi una mifumo mingapi kikubwa ni mifumo uliyonayo inakuingizia kipato kiasi gani.

Jinsi ya kutengeneza mfumo:

•  Tengeneza mfumo ambao unaweza kujiendesha hata wakati wewe ukiwa haupo.

•  Zaidi angalia kwenye tatizo lililopo kwenye jamii na uwaletee sulihisho la kudumu.

•  Kama ni tatizo angalia lisiwe tatizo ambalo ni la muda fulani na litaisha, matatizo ya kudumu ni kama afya, huduma za usafiri, maji, elimu, nishati, matatizo yako mengi sana kwenye jamii yako angalia mwenyewe na uvumbue mfumo wa kukutengenezea pesa kila siku.

•  Mfumo wowote ule unaweza kuanza nao chini kabisa hadi ukakua na ukaweza kujiendesha wenyewe.

•  Mfumo wa kukuingizia pesa ni kama mtoto anapozaliwa hadi kua mtu mzima,

•  Mtoto akiwa amezaliwa hadi kufikisha miaka 5 anakua chini ya uangalizi mkubwa wa wazazi wake,

•  Miaka 5 na kuendelea atakua karibu na mwalimu wake na wanafunzi wenzake.

•  Akifikisha miaka 18 anakua huru kujiendeshea maisha yake mwenyewe.

•  Hivyo pia mfumo wa utajiri unajengwa na kulelewa kama mtoto hadi uweze kusimama wenyewe.

•  Miaka inaweza kua tofauti lakini malezi ni yaleyale  biashara inapokua changa inahitaji uangalizi mkubwa sana wa yule mwanzilishi wake.

•  Mtoto aanapokua na umri wa siku moja hadi mwaka mmoja sio rahisi mama amwache ache hovyo mtoto.

•  Hivyo hivyo na kwenye biashara changa inahitaji uangalizi wa karibu sana kutoka kwako wewe mwanzilishi.

•  Biashara nyingi zinakufa kwa kukosa uangalizi wa karibu wakati zinakua.

•  Angalia na itunze vyema kwa faida ya baadae kama ni ya kudumu milele iweze kusimama vyema bila kuyumbishwa.

•  Unaweza kutafuta namna ya kuanza bila kua na mtaji mkubwa sana ili ukuze kidogo kidogo.

•  Kama ilivyo kwenye kulea watoto unapojifungua mapacha  watatu gharama ya kuwalea ni kubwa kuliko anapokua mmoja kama huna kipato cha kutosha watoto wanaweza kupata maradhi mengi.

•  Hivyo kama wewe ndio unaanza kumiliki biashara anza na moja ikuze hadi ianze kutembea yenyewe.

•  Hadi itakapoanza kukupa matumaini ya kuendelea mbele ndipo uanze kukuza wazo jingine.

•  Kumbuka: “Utajiri sio kua na pesa nyingi benki bali ni kua na vyanzo vingi  vinavyopeleka pesa benki.” – Jacob Mushi.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading