Vitu Vigumu/Kazi Ngumu.

By | June 22, 2016
Kuna kazi ngumu au vitu vigumu vya aina mbili vinavyotumia ubongo na vinavyotumia misuli.

Ukiniambia nikuchagulie kitu cha kufanya ili ufanikiwe nitakuonyesha kazi au idea ambayo utatumia akili/ubongo wako zaidi kuliko utakavyotumia misuli yako.

Vitu vigumu vinavyoyumia ubongo tunasema ndio vina mafanikio kwasababu ni vitafanya ubongo wako ufikiri sawasawa.

Vitu vigumu vyenyewe sio vile ambavyo kila mtu anaweza kufanya mfano “kupasua mawe makubwa, kuchimba mashimo, kubomoa kuta,  hizi ni aina ya kazi ngumu lakini sisizotumia akili. Ili uweze kupasua jiwe kubwa zaidi huendi kutafuta kitabu bora ili uongeze ufahamu wako juu ya mawe bali unaenda kula ugali wa nguvu. Kama kitu unachofanya unatumia misuli yako kwa asilimia kubwa  kuliko akili kufanikiwa itakua ngumu sana. Matokeo ya hicho kitu hayana manufaa makubwa kwenye baadae(future) yako.

Katika kuchagua biashara au kitu cha kufanya ili uingize kipato lazima uangalie misuli yako na akili zako zinatumika kwa asilimia ngapi ndipo ufanye maamuzi.

Wako watu wanafanya kazi kwa bidii sana lakini maisha yao hayabadiliki kwa kua wanatumia nguvu nyingi sana kuliko akili miili yao inachoka wanatoka majasho mengi lakini kipato kinaishia kwenye kula na anarudia pale pale.

Kama Unafanya kazi yeyote ngumu inayotumia misuli zaidi tafuta muda uwe unatulia chini na utafakari ni jinsi gani unavyoweza kusonga mbele.  Ni jinsi gani utapunguza kutumia nguvu uanze kutumia akili zaidi.

Ukisikia mtu anakwambia hii biashara ngumu muulize je ugumu wake uko wapi natakiwa nitumie nguvu kubwa ya misuli au akili yangu kufikiri. Kama unatumia akili kufikiri nenda kafanye itakufanya ukue zaidi itakufanya upige hatua mbele.

Ufanye ubongo wako ufikiri.

Ufanye nini ili utoke hapo ulipo?

Una changamoto ya kufanya vitu kwa muda mrefu bila mafanikio yeyote?

Uko pale pale kila siku?

Unatafuta biashara ya kufanya hujajua ufanye nini?

Chukua Mawasiliano yangu Tuwasiliane nikushauri.

Karibu sana
Mwandishi: Jacob Mushi
Mawasiliano: 0654726668
Email: jacob@jacobmushi.com

Jiunge na Group la WhatsApp Tuma majina yako kwenye 0654726668.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *