491; Waache Waondoke.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Kuna aina ya watu wanaweza kuja kwenye Maisha yako na kusababisha upoteze kabisa muelekeo wa Maisha. Kile ambacho umekuwa unakipigania na kukisimamia kikaanza kushuka na kupotea. Ni vyema kuwatambua watu wa namna hii mapema kabla hawajachukua nafasi kubwa na kukufanya uwe mtumwa kwao na kusahau kile ambacho ulizaliwa kuja kufanya hapa duniani.

Wapo waliongia kwenye mitego hii na sasa wanajuta hawawezi tena kutoka kwasababu wamekuwa watumwa. Wanatekeleza kila wanachoambiwa na wale waliowapokea kwenye Maisha yao. Nakusihi Rafiki yangu Maisha yako usimkabidhi mtu mwingine. Beba majukumu ya Maisha yako mwenyewe. Hata kama unajiona kama unashindwa usikubali kuuza uhuru wako. Usikubali kutoa nafasi ya kuendesha Maisha yako iende kwa wale wasiojali lile kusudi la Mungu aliloweka ndani yako.

#MUHIMU

Kuwa Makini uweze kuwatambua wale watu ambao ukikaa nao unaanza kusahau wewe ni nani, unasahau ndoto zako, malengo yako, na unajikuta umeanza kufanya yale wanayoyafanya wao.

Mara nyingi watu wa aina hii wana uwezo wa kudhibiti maisha yako. Wana uwezo wa Kukurudisha kwenye tabia zako za zamani ulizotumia muda na nguvu nyingi kuziacha.

Kaa Mbali sana na watu hawa kwasababu wanaweza kuwa Chanzo cha wewe kupoteza muelekeo wa Maisha yako.

Watu hawa wanaweza kuwa ni marafiki zako mliosoma zamani. Watu ambao wanafahamu siri zako au mambo mabaya uliyoyafanya na pia watu wanaoujua udhaifu wako.

Usikubali hata kidogo wakuendeshe, waweke mbali na wewe ili uweze kusonga mbele.

Nakutakia Kila la Kheri.

Rafiki Yako Jacob Mushi.

#usiishienjiani

www.jacobmushi.com/coach

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading