Walioshindwa jambo na wakaliacha kabisa bila kurudia au kujua kwamba wao wanahusika vipi katika kushindwa kule, wana maelezo ya kutosha kukushawishi na wewe kwa nini utashindwa.

Jihadhari sanaa na watu hawa maana wana uwezo mkubwa wa kuondoa hamasa yako juu ya jambo unalotaka kuliendea.

Waelewe hivi:
Walishindwa kwasababu ya uelewa wao mdogo juu ya jambo lile.
Wewe hakikisha una taarifa za kutosha juu ya unachokiendea.

Wana uwezo mdogo.
Wewe una uwezo mkubwa.

Alishindwa yeye sio wewe.
Wewe ni wewe usijifananishe na Walioshindwa.

Kama kile unachokifanya kuna wengine wanafanya na wamefanikiwa wewe Unaogopa nini? Waangalie washindi maana wana taarifa za kutosha juu ya kushinda kwao na watakueleza.

Walioshindwa wana taarifa za kutosha juu ya kushindwa kwao. Wana kila sababu ya kuelezea kwanini Haiwezekani. Kaa nao mbali hawa.
Wasiwe maadui lakini uwape mipaka tu ya kukueleza baadhi ya mambo.

Watu hawa wanaweza kua ndugu zako wa karibu. Labda ni wazazi wako, marafiki zako wa karibu, mke/mume,  mchumba. Unawezaje kuwaepuka watu hawa?  Kwanza Tambua wewe sio watu hawa wewe ni wewe,  wewe sio mke wako au mume wako, wewe sio mama yako au baba yako, wewe sio huyu mchumba wako. Una uwezo mkubwa sana ndani yako na wa kipekee. Huwezi kuwaacha hao watu cha msingi ni usiwape nafasi ya kuzungumzia kile unachokifanya maana wataharibu hamasa yako. Kama mtu hawezi kukupa sapoti hata ya maneno yeye anakueleza jinsi unavyokwenda kupoteza pesa zako unavyokwenda kupata hasara kubwa mtu huyo usimpe nafasi hiyo ya kuzungumzia jambo hilo maana maneno yana nguvu kubwa sana katika kuharibu au kujenga.

Wewe ni mshindi na unaweza kufanya chochote unachotaka kufanya.

Nakutakia Kila la Kheri.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading