Wateja Hawa wanakupotezea Muda

jacobmushi
2 Min Read
Habari za leo Ndugu natumaini unaendelea vyema na majukumu yako. Ninachofahamu ni kwambakila mmoja kuna kitu anauza hata kama umeajiriwa unauza ujuzi wako kwa mwajiri wako. Lakini leo nakwenda kuzungumzia juu ya wateja na changamoto walizonazo.
 
Mteja anaekwambia kwamba atachukua au ataanza bila kuweka Commitment yeyote ya tarehe au siku ambayo atachukua bidhaa au kuanza kitu fulani, mara nyingi hua hawafanyi kile walichosema na mara zote ukiwafuatilia watakwambia nikiwa tayari nitakushtua na ni mara chache sana wanakuwaga tayari.
 
Hivyo wewe kama muuzaji hakikisha mteja wako anapoahidi kitu anaweza na tarehe ya kutimiza ahadi yake. Bila hivyo unaweza kujikuta unapoteza muda wako kusubiria wateja waliokuahidi watachukua bidhaa wakiwa tayari huku mambo yako yakikwama.
Badala ya kusubiria wateja waliokwambia watachukua wewe waandike kwenye daftari lako kama alisema tarehe ya kuchukua iandike ili umfuatilie. Kisha wewe endelea kutafuta wateja wengine wapya la sivyo utajikuta unapoteza muda mwingi kuwafuatilia wateja ambao watakuumiza kichwa na kufanya uione biashara ni ngumu sana.
Pia usiache kujifunza mbinu mbalimbali za kuwafanya wateja wako wachukue bidhaa yako mapema bila kuairisha. Wakati mwingine hakikisha umefahamu changamoto inayomfanya mtu aairishe kuchukua bidhaa yako kisha unaweza kumpatia suluhisho au njia mbadala ya yeye kupata kile alichokitaka.
 
Kumbuka: Lengo kuu kwako ni wewe kutatua tatizo la mteja wako kwa kumuuzia kile unachokiuza. Lakini Biashara yako ili ikue ni kuhakikisha unauza kwa wingi Zaidi. Hivyo ni muhimu kuangalia namna ambavyo unaweza kuwauzia watu wengi na Zaidi.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
1 Comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading