Tupo kwenye dunia ambayo tulikuta watu na tutawaacha watu. Vyote tulivyovikuta vilianzishwa na binadamu wengine wenye mawazo mema na wenye mawazo mabaya pia. Vitu vingi tunavyovifanya tunaendeleza tulivyovikuta ni mara chache kukuta kitu kipya ambacho hakitegemei mazingira na asili ya tulivyovikuta. Hivyo basi kwa vyovyote vile unahitaji mtu wa kukuongoza au kuku Coach ili ufanikiwe katika pande zote za maisha.
Nitakwenda kuzungumzia sehemu kuu tatu za muhimu sana ambazo unatakiwa uwe na watu wa kukuongoza ili uweze kukua na kupanda viwango kila wakati. Ni vitu vya kawaida sana lakini leo nitakwenda kuzungumzia uone ilivyo muhimu sana wewe kua na vitu hivi maana bila vitu hivi mafanikio yatakua magumu sana kufikia. Safari yako itakua ngumu zaidi kama utakosea sehemu hizi tatu.
Nitaomba tuelewane kwamba hapa huendi kuiga au kua hawa watu utakua wewe na utatimiza lile kusudi la Mungu ndani yako.  Kwanza kabisa uko hivyo ulivyo kwa sababu ya mazingira uliyokulia na watu tulioishi nao tangu ukiwa mtoto  hadi hapo ulipo. Kuna tabia nyingi sana unazo kutokana na mazingira uliyokulia. (Hapa ndipo nakutana na kitu ambacho nakipenda sana kujifunza kwa wengine napenda kujifunza kwenye mazingira mapya na kwa watu wapya kwa kua wameishi maisha ambayo mimi siyajui na wanafahamu vitu vingi ambavyo mimi sifahamu. Watu wana utajiri mwingi sana ndani yao ukiweza kukaa na mtu ambaye humjui kabisa unaweza kujifunza mambo mengi ya ajabu kwake. )
Hawa ndio watu wa Muhimu sana kwenye safari yako usiwakose ili uweze kusonga mbele. Sifa zao kabla hujawachagua ni za muhimu sana pia ili wasije wakakupoteza badala ya kukufikisha kule unakotaka kwenda.  
(a)Awe na mafanikio (Amefika Mbali) kwenye hiyo sehemu.
(b)Awe na Tabia njema zinazokubalika na jamii yake na dini yake. (mfano hapa ukikutana na mtu ambaye anakuelekeza kuhusu biashara na ni mlevi na mzinzi hizi tabia lazima atakuambukiza kwasababu atakua mtu wako wa karibu sana)
(c)Awe amekuzidi  sana kwenye kile unachotaka akulelee (akuongoze). 
Hizo ni sifa za muhimu tu za kuangalia zipo nyingine nyingi sana utajifunza mwenyewe.
1. Mlezi wako wa Kiroho
Huyu ni mtu wa muhimu sana na nimemweka wa kwanza.
Bila roho hakuna mwili
Bila roho mwili wako unakua umekufa.
Unahitaji ukue kiroho na upande viwango kila wakati. Ili uweze kuvutia mafanikio ya nje.
Ukishindwa hapa hata ukiwa bilionaire inaweza kua kazi bure.
Hutaweza kuzifurahia.
Tafuta mtu wa kukulelea kiroho.
Mtu wa kukufundisha kumcha Mungu.
Kama huna katafute mtu wa kukulea kiroho sifa nimezitaja hapo juu.
Mtu huyu anatakiwa akufahamu vizuri na wewe umfahamu vizuri.
Yaani muwe na mahusiano ya karibu sana.
Mtu huyu awe anafuatilia maendeleo yako ya kiroho kwa karibu sana.
Haijalishi uko Dini gani lazima umpate mlezi wa roho yako Dini ndio.inahusika kulisha roho zetu. Ndio maana hatufundishwi biashara kule.
2. Mlezi wa Mahusiano/Uchumba/Ndoa
Hapa ni kwa muhimu sana. Ukiwa vizuri kiroho mahusiano yakawa na tatizo hutafika mbali.
Ukiwa vizuri kiroho ndoa ikasumbua nayo ni tatizo.
Tafuta mtu wa kukulea kwa upande huu pia mtu aliefika mbele zaidi yako. Aliefanikiwa zaidi yako.
Kama unatafuta mchumba tafuta mtu alie kwenye ndoa na amefanikiwa.
Ukimtafuta single mwenzako atakupoteza?.
Mtu huyu awe karibu yenu kabisa kulea mahusiano/ uchumba au ndoa yenu.
Hakuna alie zaliwa anajua kila kitu tunajifunza hapa duniani kwa waliotutangulia na waliopo pia.
3. Mlezi wa Maono yako/Ndoto zako/Malengo yako/Biashara Yako/Pesa. (Coacher).
Mtu huyu ni wa muhimu pia katika maisha yako. Unataka kumiliki utajiri wa dollar billion moja lazima utafute mtu wa kukulelea na kukuwezesha ufikie huko. Huwezi kwenda mwenyewe.
Unahitaji mtu wa kukuongoza kwenye kila unachotaka kukifanya.
Wengi wanakata tamaa kwa kua hawana watu hawa wa kuwalelea.
Mtu huyu anatakiwa awe anakufuatilia hatua kwa hatua kwenye kile unachokifanya.
Awe anapata taarifa za maendeleo yako kila wakati ikiwezekana hata kila week.
Ukipata mafanikio yeyote ajue pia ukipata changamoto ajue.
Mtu huyu anatakiwa awe amekupita kwenye kile unachokitaka na hapa huendi kua Follower anakwenda kukutengeneza wewe uwe kiongozi. Uweze kusimama mwenyewe na hatimae uongoze wengine.
Kwa Tanzania wapo watu wanaofanya kazi hizi kwa malipo pia. Lakini hapa unaweza kuanza na mtu.ambaye una mahusiano nae ya karibu awe anakulelea.
Siku hizi teknolojia imekua rahisi sana unaweza kua na mawasiliano na mtu yeyote unaemtaka popote alipo duniani. Unaweza kujifunza pia vitu vingi sana kupitia mitandao hii kama hapa kwenye group.
Unaweza kusoma vitabu na vitu vingi sana vile.unavyovitaka.
Naomba nimalizie kwa kusema kwamba.
Kwa hiki ulichokipata leo ukikifanyia kazi Utakua mshindi ulie zaliwa kua.
Utafikia Hatma yako.
Kwa kufuata haya
Wewe namaanisha wewe iliesoma leo

I will see you at the top!
Jacob Mushi
+255654726668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading