Kila mtu kuna sehemu ambayo ni Hodari sana kuliko sehemu nyingine. Na hili ndio mojawapo ya mambo yanayotutofautisha wanadamu, unaweza kuwaleta watu kumi wanaofanya kitu kimoja ambacho kinafanana kabisa lakini unakuta kila mmoja ana sehemu ambayo yeye ni Hodari kuliko wengine.

Si vyema kabisa kumdharau mwenzako kwasababu ya kile ambacho unadhani unakijua kuliko yeye kumbuka kwamba hata yeye kuna jambo ambalo analiweza vizuri kuliko wewe labda tu hajaamua kukuonesha.

Ukiweza kutambua wewe ni sehemu ipi hasa upo Hodari unatakiwa uweke nguvu zako nyingi hapo kuliko zile sehemu ambazo ni dhaifu. Mojawapo ya vitu vinavyowatesa wengi ni kusahau kwamba huwezi kuwa kama Fulani bali unaweza kuwa wewe kwa kufanya kile ambacho wewe ni Hodari Zaidi.

Kaini na Habili kilichofanya ugomvi na chuki iamke kati yao ni kile kitendo cha mmoja kuona kama mwenzake anafanya vizuri kuliko mimi. Kama Kaini angeweza kubaki kwenye kilimo chake bila kutazama kwa jicho baya mifugo ya mwenzake basi angeweza kuleta mazao bora kwa Bwana.

Usipoteze muda kutazama wengine wanafanyaje kila kitu kipo ndani yako ujue, jitazame wewe ni Hodari kwenye nini halafu ufanyie kazi kwa bidii. Jifunze mbinu mpya na njia mbalimbali za kuboresha kile ambacho wewe ni Hodari Zaidi.

Mafanikio yako yapo kwenye kile kitu ambacho wewe ni Hodari Zaidi. Ukipoteza muda kufanya vitu ambavyo sio vyako utajikuta unatumia muda mwingi na nguvu nyingi lakini hupati matokeo makubwa.

Jiulize mara kwa mara hadi ujue na chukua hatua mara kwa mara hadi uone kile ambacho unakiweza vizuri sana. Usipoteze muda kutazama kile ambacho wewe ni dhaifu, utajikuta unapata hofu na unashindwa haraka.

 Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Kocha Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading