Wewe Ni Muujiza Uliokua Unausubiri.

Habari ya leo ndugu msomaji wetu mpendwa. Ni matumaini yangu unaendelea vyema na mipango yako ya maisha. Karibu tena leo katika makala yetu. Leo tutajifunza somo linaitwa “Wewe Ni Muujiza Uliokua Unausubiri”.Wewe ndie muujiza wako katika maisha tumezoea kumuomba Mungu nakusubiri ajibu ni kweli  anajibu lakini  lazima na wewe uhusike katika hatua za kujibiwa kuomba tu haitoshi labda kama unakemea pepo.

Pia kama unakemea pepo lazima uwe unafanya pia baadhi ya vitendo. Ukimwomba Mungu akupe gari lakini huna bidii ya kutafuta  huwezi kuamka asubuhi ukakuta amekuletea. Usiogope inawezekana kupata kile ulichomwomba Mungu ni wewe kuongeza bidii tu. Umeomba upandishwe cheo kama hubadili jinsi unavyofanya kazi kwa ubora zaidi haitakaa itokee. Kila muujiza wa maisha yetu tunahusika katika kuutekeleza.

Tufanye kazi kwa bidii tumuombe Mungu sana tudumishe mahusoano yetu na wengine kama tulivyoona kwenye makala zilizopita. Tuwe waadilifu katika kila jambo baraka za Mungu hazitaacha kumiminika juu ya maisha yetu. Mungu wetu ndie mwenye vyote vya dunia hii anaweza kutupatia lakini lazima tujihusishe katika kupokea miujiza hiyo.

Napenda nikwambie kua hujazaliwa kwa bahati mbaya haipo hapa duniani bila sababu. Mungu ana mpango mkubwa na wewe unachotakiwa ni kuona. Kufunguka ufahamu wako wa ndani uweze kuziona baraka hizo na kuzifanyia kazi.”Wewe ni Muujiza unaousubiria”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading