Kwenye dunia ya sasa kuna vitu vingi sana vinazalishwa kila siku na kila wakati vinagunduliwa vipya. Kitu kimoja kinachonifurahisha zaidi ni kwamba tuna watumiaji wengi sana ambao hawaachi kitu kipya kije bila wao kutumia.
Jiulize leo unatumia vitu vingapi na kwa faida gani? Tuanze na mitandao ya kijamii pamoja na vifaa vyake.
⚠Umenunua laini ambayo unaweka vocha kila siku na kununua MB ili utumie WhatsApp na mitandao mingine.
⚠Umenunua simu mpya ya ghali ili uweze kupiga picha nzuri na kuzituma Facebook na WhatsApp.
⚠Nyumbani una Tv, King’amuzi na Deki. Una burn cd kila siku ili uangalie movie mpya. Unalipia king’amuzi na umeme kila mwezi ili uweze kutumia na kuangalia tv.
⚠ Kila nguo mpya ikitoka unanunua. Vitu vipya vya kila aina unataka.
⚠Bado hujala chakula unanunua kila siku vyakula ili ule.
⁉Jiulize sasa ni vingapi wewe unafanya watu wanakuja kununua kwako ili wakuingizie pesa?
⁉Unapotumia mitandao ya kijamii kuchati masaa 24 unatengeneza faida gani?
⁉Ulishawahi kujiuliza jinsi wamiliki wa mitandao hii wanavyotengeneza pesa?
⁉ Hata kama unajifunza huwezi kujifunza kila saa lazima uwe na muda wa kuingia na kujifunza na muda wa kufanya mambo mengine.
Sio vibaya lakini kua mtumiaji tu wa kila tu utaishia kua maskini.
✅Ukitaka kufanikiwa na kupata faida chagua kua mtu wa katikati MZALISHAJI na Mtumiaji/MLAJI au uwe msambazaji na Mtumiaji/mlaji. Hii ndio njia ya pekee kwenye kila kitu.
? Unaweza kumiliki utajiri leo kwa kuanza kuitumia mitandao ya kijamii vizuri. Unaweza kua sehemu ya watu wanaofaidika na mabadiliko yanayotokea kila siku badala ya kua mtumiaji tu.
? Ni wakati wako sasa jifunze na uone jinsi ya kunufaika acha kupoteza muda na kulaumu eti Mambo yamekua magumu!
? Wakati wewe unalalamika hali ngumu kuna wenzako wanaagiza magari mapya. Wakati wewe uko bize unachati kwenye groups kuna mwingine anauza bidhaa ana tangaza bidhaa yake na anatengeneza pesa.
Wakati wewe upoo bize kuperuzi mitandaoni kuna wenzako wanatengeneza pesa huko unakopoteza muda wa kuperuzi tu.
Acha kulalamika chukua hatua.
Usikubali kua mtumiaji tu wa kila kitu hakikisha unazalisha zaidi kuliko unavyotumia lazima uwe na mafanikio
Rafiki Yako,
Jacob Mushi
#UsiishieNjiani