“Wewe ni nyota popote pale ulipo hakikisha unang’ara” Jacob Mushi 2018. Mwaka huu haijalishi upo sehemu gani unafanya kazi ya aina gani bado unahitajika kuonyesha kile kilichopo ndani yako.
Haijalishi unaishi Maisha ya hali gani bado unatakiwa kuendelea kuonyesha kwamba wewe ni wa thamani. Dhahabu ikitupwa kwenye takataka bado inaendelea kubakia ni dhahabu. Haibadilishwi na mazingira.
Popote pale ulipo ili uweze kuinuka na kutoka hapo ulipo ni muhimu sana ukaonyesha wewe ni nani. Fanya kwa bidi sana kuonyesha kile ambacho Mungu ameweka ndani yako Zaidi.
Hata kama nyota imewekwa chini ya uvungu ili iweze kujulikana kuna nyota chini ya uvungu ni nyota ile kung’ara hapo tu ndio watu watafanya jitihada za kuitoa kwenye uvungu na kuiweka juu. Kile kilichopo ndani yako ukikifunika utapotea kabisa.
Ukiendelea kusema unasubiria sehemu nzuri ya kuonyesha kile ambacho unacho utakuja kujikuta unaendelea kutumbukia kwenye shimo na usionekane tena. Onyesha kile kilichopo ndani yako sasa hivi bila ya kuogopa.
Tai akiogopa kuonyesha kwamba yeye ni Tai kwasababu tu kawekwa na kuku hakuna atakae jua kwamba hapa kuna tai. Lazima kwanza tai aonyeshe tofauti yake mbele ya kuku kwa kuruka juu Zaidi.
Natamani mwako 2018 uwe ni mwaka wako wa kung’ara na kuonekana. Chochote utakachokigusa watu wajue kwamba hapa kuna mtu wa tofauti amepita.
Usiogope na wala Usikubali Kuishia Njiani.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,
Simu: 0654 726 668,
Twitter: jacobmushitz
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page
Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com