Umekutana na mtu ukatamani sana kuzungumza nae lakini ghafla yakaanza kuja mawazo kichwani kwako kwamba, “huyu atakuwa anaringa” “mimi sistahili” “nitaongea nae siku nyingine”. Mwishoe unaondoka huku ukiwa hujaweza kuzungumza neno lolote. Huu ni woga na hofu ambayo umejitengenezea mwenyewe. Kwanza unatakiwa ujue hata kama hayo unayowaza ni ya kweli basi yeye ndie ana matatizo sio wewe. Hivyo jivike ujasiri nenda zungumza.

Ukiwa katikati ya pori ukakutana na simba haijalishi utakuwa na woga kiasi gani hautakusaidia chochote. Kitu pekee ambacho kinaweza kukusaidia ni ujasiri. Hata kama ungelia na kutokwa na machozi simba hawezi kukuhurumia, ila ukiweza kuonesha kwamba huogopi chochote basi angalau itampa woga kidogo simba.

Unaogopa kufa na bado unakufa, haina maana yeyote ya wewe kuendelea kuogopa kifo. Unaogopa kupata hasara kwenye biashara unaanza na unapata hasara, woga wako haujakusaidia chochote. Ujasiri ndio unaweza kukuongezea hata nafasi ile ya kuchukua hatua.

Ukiogopa hakuna kitakachobadilika. Ukiogopa kupata hasara hakuna kitakachobadilika Zaidi hali itakuwa mbaya Zaidi. Unapaswa uelewa kwamba lolote ambalo litatokea ni sawa kwasababu lipo nje ya uwezo wako.

Woga utakucheleweshea muda wa kuanza kile ambacho unasema unataka kuanza.

Woga utaendelea kukufanya uendelee kuahirisha kila mara.

Woga utakufanya urudi nyuma badala ya kusonga mbele.

Woga utakukosesha vitu ambavyo ilikuwa ni haki yako kabisa kupata.

Woga ni majibu ambayo umejipa wewe lakini sio majibu ya kweli.

Woga unakunyima vitu vizuri hata vile ambavyo ulistahili kabisa.

Tengeneza tabia ya kuchukua hatua kwenye vitu vidogo vidogo hasa vile ambavyo vinakupa hofu. Jione wewe ni mshindi, kaa na watu ambao wana hamasa, na wanaochukua hatua. Jifunze kwa wanaofanya mambo makubwa. Ondoa woga kidogo kidogo kwa kujaribu kile ambacho kinakupa hofu mara kwa mara.

Ukiona kuna jambo unaogopa kufanya basi hilo ndio jambo unalotakiwa kufanya.

Acha woga, Kuwa Jasiri, Chukua Hatua.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading