513; Bwana Yesu Asingesema Kuwa Atarudi Tena Ingekuaje?

jacobmushi
3 Min Read

Heri Ya Mwaka Mpya, naamini umevuka salama kabisa .

Leo nimekuwa nawaza kitu hapa, cha ajabu sana ila utanisamehe kama utaona naenda nje ya misingi yako ya kuamini na kuwaza juu ya Imani.

Unajua kuna vitu vingi ukivitafakari kwenye maisha unajikuta unapata picha toafauti ambazo watu wengi hawawezi kuziona kirahisi.

Nimejiuliza kwamba mfano Bwana wetu Yesu kabla ya kupaa aliwaambia wanafunzi wake wasifadhaike mioyoni mwao kwani atarudi tena.

Sasa nimekaa nikiwaza ivi kama angeondoka bila ya kutoa ahadi yoyote ingekuaje? Je imani ingekuwepo mpaka sasa?

Wakati unaendelea kutafakari na wewe nataka ujue kwamba mimi pia naamini atarudi, usije kusema huyu jamaa ameshakata tamaa.

Nikawaza kwa undani zaidi kwamba kinachotufanya tuendelee kuwa na imani kwamba atarudi ni ile ahadi ambayo ametuachie kwamba atarudi tena.

Pata Vitabu vya Maarifa Bonyeza Hapa

Tukirudi nyuma kidogo kule Jangwani wale wana wa Israel walikata tamaa mapema sana baada tu ya Musa kuchelewa kurudi kule Mlimani na kuanza kutengeneza sanamu ya ndama. Hawa watu tukiwatazama tunaona walikosa matumaini.

Nataka nikwambie kwamba kitu pekee kinachoweza kufanya uendelee kuishi kwa imani katika kusudi lako ni ile imani kwamba ipo siku utafika sehemu fulani kubwa.

Kama huna maono yoyote makubwa lazima utafika mahali na kuona kama unafuata kitu ambacho hakipo.

Sasa kama Bwana Yesu aliondoka miaka elfu mbili iliyopita na mpaka sasa kuna watu tunaendelea kushikilia Imani na tukiamini kwamba anarudi Tena, kwanini wewe unataka kukata tamaa kwenye ndoto yako kubwa?

Kwanini basi hujakata tamaa kumsubiri Yesu? Yeye mwenyewe anakusubiri wewe umalize kile ulichokuja kufanya hapa duniani.

Rafiki nataka nikwambie, unajua ni kwanini watu wanaendelea kuamini kwamba Yesu anarudi siku sio nyingi? Kwasababu wiki moja haipiti bila ya bila ya kuabudu. Wewe zinapita siku ngapi hujapitia yale maono yako?

Inawezekana huwa unayapitia mwanzoni mwa Mwaka, katikati ya mwaka na mwishoni mwa mwaka. Sasa jiulize mtu ambaye anakwenda kanisani mara tatu kwa mwaka hali yake ya kiimani ikoje? Atakuwa na matumaini kweli?

Sasa kama na wewe unakosa muda wa kukaa na wenzako mnaoamini katika kitu kimoja, unakosa kusoma vitabu, unakosa kupitia maono na ndoto zako mara kwa mara, ni rahisi sana kupoteza matumani.

Nimeandika kitabu cha Usiishie Njiani, na pamoja kuendesha kampeni ya Usiishie Njiani kwa ajili ya kukusaidia wewe usije kukata tamaa katika yale maono makubwa uliyonayo.

Ili usiishie njiani unahitaji kuwa na maono makubwa ambayo unayaishi kila siku, kama ambavyo tunakwenda ibadani kila wiki, tunasali kila siku, hivyo pia na wewe unatakiwa uweze kujitoa kiasi hicho kwenye maono yako.

Tunakwenda kuabudu tukiamini na tukitarajia kitu kizuri kikubwa baada ya Maisha haya. Na wewe binafsi unapaswa kutarajia pia Maisha bora Zaidi ya hayo unayoishi sasa hivi kwa zile bidi unazoweka kwenye kazi zako.

Naamini hutakata tamaa kirahisi,

Usiishie Njaini

Rafiki Yako

Jacob Mushi.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
6 Comments

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading