Habari za leo Rafiki yangu? Unaendeleaje na Maisha? Natumaini unaendelea vyema sana.
Nina zawadi nzuri sana nimekuandalia ndani ya mwaka huu 2017 mojawapo ya zawadi hizo ni kuchapisha kitabu nilichoandika kwa ajili yako. Kitabu hiki kitakuwa ni zawadi ya kwanza ambayo nitaanza kukupatia mwezi wa February. Kitabu hiki kimebeba mambo saba ya muhimu ambayo unatakiwa kuyafahamu ili uishi Maisha yenye maana hapa duniani.
Kitabu hiki nimeandika kwa ajili yako wewe Rafiki yangu. Ukikisoma utakutana na mambo mengi ya muhimu kwenye Maisha yako. Maisha yako yamebebwa na hizi siri utakapozitambua na kuzifanyia kazi Maisha yanakwenda kuwa bora sana.
Hii ni zawadi ambayo utailipia gharama kidogo sana kulingana na kile ambacho kipo ndani yake. Kitabu hiki kitauzwa kwa Tsh 10,000/= shilingi elfu kumi tu. Ninataka uweke oda yako mapema ili visije kuisha kabla hujapata nakala yako. Watu wanaohitaji kitabu hiki ni wengi sana hivyo na wewe ukijitokeza utanipa nafasi ya kujua kama naongeza idadi ya nakala.
Muda bado upo unaweza kuweka oda yako mapema. Mwaka huu 2017 ukiwekeza katika kusoma vitabu Maisha yako yatakuwa ya maana sana na yenye mafanikio makubwa.
Haijalishi upo mkoa gani kitabu kikitoka utakipata kwa njia rahisi sana. Karibu sana ujipatie maarifa haya Maisha yako yawe na alama hapa duniani.
Haya ndio mambo ya pekee yaliyopo ndani ya kitabu hiki:
1. Tambua kwanini upo Hai Leo na uweze kutumia nafasi hiyo kutengeneza Historia mpya ndani ya Dunia hii.
2. Kuna mambo mengi tunayafanya, kupitia Siri hizi utaweza kutambua kwanini unatakiwa umalize ulichokianza.
3. Kwenye Siri 7 pia utajifunza namna ya kutengeneza ulipoharibu. Kuna makosa mengi umefanya katika maisha yako, umewaumiza wengi kwa kujua na kutokujua. Hapa utaweza kujua namna ya kutengeneza upya.
4. Kulitambua kusudi lako la kuwepo duniani. Hakuna mwanadamu aliyeko bila sababu. Kila mtu yupo kwa kusudi maalumu hivyo utaweza kutambua namna gani ya kujua kusudi lako na kuendelea kuliishi hadi ufikie utimilifu.
5. Utajifunza namna ya kutumia zawadi zilizopo ndani yako. Upekee uliozaliwa nao, nguvu ya kuvumbua mambo mbalimbali kutokana na kile unachokifanya.
6. Utajifunza jinsi ya kugusa maisha ya wengine kupitia kile unachokifanya. Kwani kwa kugusa maisha ya wengine ndiko Kwenye utajiri na kila kitu tunachokitafuta hapa duniani.
Usikubali kukosa nakala yako yapo mengi sana ya kujifunza ndani ya kitabu hiki. Kupata Kitabu hiki wasiliana nami kwa namba 0654726668 .
Karibu sana tufanye kazi pamoja.
Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com, www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.