Habari rafiki, ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema kabisa. Na ninaamini pia unaendelea kupambana ili kuifanya ndoto yako kuwa kweli. Usiogope wala usikate tamaa hakuna kitu kizuri chenye thamani kubwa kinachopatikana kirahisi. Endelea mbele.

Kama tunavyojua mafanikio ni tabia, vilevile kutokufanikiwa ni tabia. Kama kuna tabia ambazo zinaweza kufanyika sababu ya watu Fulani kufanikiwa pia zipo sababu zinazofanya wengine wasifanikiwe. Leo tutajifunza tabia 5 ambazo zimekuwa changamoto kwa vijana wengi kushindwa kufikia mafanikio yao.  Ukiweza kukaa mbali na tabia hizi haijalishi upo kwenye hali gani sasa mafanikio ni lazima utayafikia kwneye kile unachokifanya.

1. Kupenda Fedha za Haraka.

Vijana wengi wamekuwa na tabia za kupenda fedha au mafanikio ya haraka haraka, hivyo kujikuta wanafanya vitu visivyofaa ili tu wapate fedha. Kama tabia hii itakuwa ndani yako huwezi kufika sehemu yeyote ile. Hata pesa utakazopata bila ya kuzitolea jasho zitapotea kama upepo.

Fedha inayodumu kwa yule aitafutaye ni fedha ambayo imepatikana katika njia halali. Tunaposema njia halali ni njia zote zile zinazoongeza thamani kwa wengine.

Usipoteze muda wako sehemu ambayo hutumii bidi yako au huweki juhudi zozote. Ukweli ni kwamba fedha unaweza kuzipata lakini hazina thamani, huwezi kuja kuwa mfano mzuri hata kwa watoto wako mwenyewe. Tamaa ya pesa za haraka ni mbaya sana na inakupotezea muda wako.

Wekeze kwenye akili yako, soma vitabu fanyia kazi yale unayojifunza ili ufikie mafanikio. Kama zingekuwepo njia rahisi za kupata pesa na za halali watu wa kwanza kuzichukua wangekuwa matajiri wakubwa. Hivyo usijidanganye mwenyewe.

2. Kudharau wengine.

Tabia ya kuonyesha dharau kwa wengine ni mbaya sana. Umepambana ndio umeanza kufanikiwa kidogo yaani pesa ndio umeanza kuzishika shika hivi. Bahati nzuri Zaidi ukaweza kununua na usafiri wako sasa umefikia hatua hata husalimii wengine. Unawaona ni wajinga wale ambao umewapita kimafanikio.

Watu wenye mafanikio hawana dharau kwa wengine kwasababu wanajua tunategemeana kwa vitu mbalimbali. Wewe una gari usimdharau fundi simu ipo siku utamhitaji. Umeajiajiri usimdharau mwalimu ipo siku utamhitaji afundishe watoto wako.

Soma: Uvumilivu ni Muhimu

Umefanikiwa kufungua kampuni yako usimdharau daktarin ambaye bado yupo kwenye ajira ipo siku utamhitaji kwa ajili ya matibabu. Ona kazi njema walizonazo wenzako hata kama ni mama muuza mahindi ya kuchoma barabarani. Ipo siku atakuja kuwauzia watoto wako.

Mheshimu kila mmoja unaekutana nae hujui ni wapi utakuja kumhitaji. Inawezekana wewe unajiona umesoma sana labda ni mwanasheria nguli sana. Lakini unamdharau mtu ambaye hajasoma kesho unapita na gari barabarani unapata pancha uliemdharau ndie fundi pancha.

3. Tamaa Mbaya.

Vijana tunapenda starehe, tunatamani Maisha ya hali ya juu. Hii inakuwa tatizo sana kama utaanza kuwa na tamaa ya Maisha ambayo hujayafikia. Biashara yako haijakua vya kutosha unataka kila mtu ajue wewe ni bosi. Utaanza kubadilisha sehemu uliyokuwa unakula.

Utaanza kubadilisha hadi usafiri ili uonekane bosi wakati biashara haijasimama. Ni hatari sana kwani unaowaonyesha hawakusaidii chochote.

Ukifikia sehemu ambayo unaanza kuona kila starehe unataka ujue umeanza kupoteza dira. Kwa mafanikio madogo uliyopata usikubali tamaa ikupeleke pabaya. Vijana wa kiume wataanza tabia za kuhonga na kubadilisha wanawake, mwisho wa siku biashara inakufa na wewe unafuatia kuugua na magonjwa.

Tamaa mbaya ikae mbali na wewe kama unayataka mafanikio ya kweli. Vitu vyote vinavyokuletea raha za muda mfupi achana navyo. Usipende kumwonyesha mtu yeyote kwamba una mafanikio Fulani acha waone wenyewe.

4. Kiburi

Tabia ya kiburi inaambatana na dharau. Ukishakuwa na kiburi maana yake ni kwamba lazima uanze kuwadharau wale wanaojaribu kukuelekeza na kukuonyesha njia. Ukiona umefikia mahali unawaona wanaokushauri wanakuonea wivu ujue umeanza kupotea.

Usikubali kulewa kiburi cha mafanikio madogo uliyoanza kuyapata utaishia pabaya sana. Na huko pabaya ni kupoteza kila ulichonacho. Itakuwa ni aibu sana kwani wale uliowaonyesha kiburi inawezekana wakawa ni watu ambao unatakiwa uwafate wakushauri tena.

Endelea kuwa mnyenyekevu kama kipindi kile ulipokuwa huna kitu. Usitafute sifa zisizo na maana wacha watu wakusifie wenyewe na usipokee sifa maana zinalewesha zirudishe kwa Mungu sifa zote.

Soma: Kubali Wanayofanya Wengine

Mafanikio yanakwenda kwa watu wenye uadilifu wanaoweka juhudu na kujituma. Wote walionyesha kuwa wao ndio wanajua wameishia pabaya. Endelea kujifunza kwani hata tajiri wa kwanza wa dunia anajifunza kila siku sembuse wewe?

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Mwandishi, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

2 Responses

Leave a Reply to Jacob MushiCancel reply

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading