537; Ingia Ndani Zaidi..

Watanzania wengi ni wavivu sana kusoma, kabla hujaamini picha ya kichwa cha habari inayosambazwa jaribu kutafuta habari nzima uisome na uelewe. Vichwa vingi vya habari huandikwa kwa namna ya kuvuta wasomaji na bahati mbaya sana wengi wenu huishia kusoma kichwa tu na kufikia hitimisho. Usiwe mwepesi pia kuamini kila kilichoandikwa kwasababu kwenye ulimwengu wa sasa… Read More »

536: Huwezi Kuwaridhisha.

Watu wanaweza kukuchukia pasipo na sababu yoyote ya msingi. Inawezekana hata hujawahi kuwasemesha lakini wakakuchukia. Inawezekana hujawawahi kuwatendea jambo lolote lile baya au la kuudhi lakini wakakuchukia tu. Unapaswa tu kutambua kwamba hata ufanye mambo mema kiasi gani hapa duniani huwezi kupendwa na kila mtu. Huwezi kumridhisha kila mtu. Unaweza kuzungumza sentensi moja ikamsaidia mtu… Read More »

534: Ni Nini Kitafuata?

Miaka michache iliyopita kuna vingi vilivyogunduliwa kipindi hiki havikuwepo kabisa na vingine hata havikudhaniwa kama vingewezekana. Kilichofanya haya mambo makubwa tuyaonayo sasa yaweze kutimia ni kile kitendo cha watu kutaka kujua wanawezaje kuleta suluhisho kwenye jamii. Ni muhimu sana kama unataka kuwa mmoja wa watu ambao wataleta mabadiliko kwenye dunia hii basi uweze kujiuliza swali… Read More »

532; Uliza.

Shida kubwa tuliyonayo watu wengi ni kujipa majibu ya maswali ambayo tunajiuliza wenyewe kuhusu watu wengine. Mara tu unapoingiwa na wasiwasi kichwani mwako juu ya jambo fulani usiishie kujipa majibu mara nyingi utajikuta unajipa majibu ya uongo. Unapojikuta kwenye wasiwasi wa jambo fulani ndani ya akili yako usikubali kujipa majibu mwenyewe ULIZA SWALI. Unapouliza ndio… Read More »

Mafanikio ni Mchakato.

Nilipokua sekondari tulitumia barabara mbaya sana kuelekea shuleni kitu kilichofanya safari iwe ya kuchosha sana na yenye kuchukua muda mrefu sana.Kipindi hicho barabara nzuri ya lami ilikua ikitengenezwa, kila nilipokua nikisafiri kwenda na kurudi shule nilitumia muda huo kujifunza juu ya ujenzi wa barabara! Ujenzi wa barabara unapoanza unaudhi sana kwani miti hukatwa , udongo… Read More »

Haijalishi Umezaliwa Wapi, Maisha ni Zawadi.

Katika maisha haya kamwe usimlaumu mtu yeyote kwasababu ya kushindwa kwako au kufeli kwako jambo fulani, kwasababu kulaumu hakuibadilishi hali bali kunatengeneza tatizo lingine linaitwa KiNYoNgO. Hakuna mtu aliyetuma barua ya maombi kwa MUNGU azaliwe katika familia fulani yenye hali fulani au uzuri fulani, Wote tumezaliwa tumejikuta watoto wa fulani na fulani, Wengine wamezaliwa wamejikuta… Read More »