HATUA YA 72: Sheria ya Uvutano.

jacobmushi
2 Min Read
Kuna sheria nyingi za asili ambazo zinayaongoza maisha yetu kila siku ila wengi wetu tumeshindwa kujua namna ya kuzitumia ili kuwa na maisha bora.
Sheria ya uvutano ni mojawapo ya sheria hizi. Kikawaida chuma kinavutwa na chuma mwenzake. Sumaku inavuta chuma haiwezi kuvuta mbao au kitu kisichokuwa na asili ya chuma.
Hivyo kwenye maisha yako vile ulivyonavyo vinatokana na jinsi wewe mwenyewe ulivyo. Ukiwa na mwenzi ambaye unafikiri ana tabia mbaya jitazame kwanza tabia zako maana huwezi kuvutia kitu ambacho hakifanani na wewe.
Marafiki ulionao wanafanana na wewe kabisa. Angalia tabia walizonazo kama haziendani na za kwako. Hata kama sio zote basi kuna tabia fulani ilianza kuwavuta pamoja, mwisho wa siku mnakuta mmeshaigana tabia zote.
Ni muhimu sana tukatambua hili ili tuweze kuwa na maisha yale tunayoyataka.
Ili uweze kupata chochote unachokitaka unatakiwa uanze kubadilika ndani.
Tabia ya uvivu inavutia umaskini.
Tabia ya kutokuweka akiba inavutia kuwa na madeni mengi.
Tabia ya kutokusoma  Vitabu inakuletea kushindwa kwenye mambo mengi kwasababu unakuwa huna taarifa za kutosha.
Kama unataka marafiki ambao wana mtazamo chanya anza kuwa na mtazamo chanya kwanza.
Unataka marafiki wenye pesa na wanaowaza mafanikio anza kuwaza mafanikio kwanza.
Unataka kuoa/kuolewa na mtu mwenye tabia fulani unazotaka anza kuwa nazo wewe mwenyewe.
Chochote unachokitaka kwa wengine anza kuwa nacho wewe utakipata.
Unawavutia watu kutokana na jinsi ulivyo wewe.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
1 Comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading