?Kwanini mshahara haukutani?
?Kwanini kipato hakitoshelezi mahitaji?
?Unalipa kwa watu wengi kuliko unavyo lipwa!
?Unawapelekea watu wengi kuliko wewe unavyoletewa pesa!
?Wewe mwajiriwa!
Unalipa kodi Serikali kabla hujapokea mshahara!
Unalipa bima ya afya kabla mshahara haujakufikia!
Unalipa kodi ya nyumba!
Unalipa bili ya umeme na maji!
Unalipa ada ya mtoto au wadogo zako!
Unamlipa muuza vocha!
Unamlipa muuza chakula!
Unamlipa muuza nguo!
Unamlipa konda nauli!
Unamlipa dereva wa bodaboda!
Kama ni mwanaume bado hujamlipia mpenzi wako vitu kadhaa sivitaji!
Endelea kujiangalia ni vitu gani unalipa kila siku halafu angalia wewe unalipwa nini?
⁉WEWE UNALIPWA MSHAHARA TU!‼
Ukweli mshahara hautakaa utoshe. Ongeza njia nyingine za vipato na punguza vitu unavyolipa visivyo vya maana.
Upo tayari kuendelea na hali hiyo miaka 40? Maisha yako utayabadili mwenyewe hakuna mtu mwingine anaweza kubadilisha maisha yako!
Zitumie vizuri fursa unazokutana nazo kwa sababu hakuna namna nyingine. Dunia inabadilika na mabadiliko makubwa yanakuja kila siku.
Ni wakati wako kubadilisha hali usiyoitaka kwenye maisha.
Usiniambie huna mtaji tatizo sio mtaji tatizo ni wewe. Kama huna mtaji una mpango gani wa kuupata? Maana kusema huna mtaji matatizo hayatakuhurumia. Lazima ukubali kutafuta njia ya kutoka hapo ulipo!
Hakuna wa kumlaumu juu ya matatizo yako zaidi ya wewe mwenyewe. Sio Serikali wala mzazi wala elimu mbovu.
Nina amini ukiamua kubadilisha maisha yako unaweza. Anza kujiamini. Fanya kazi kwa bidii jifunze sana acha kufuatilia vitu visivyo na msaada wowote
Rafiki Yako Jacob Mushi