Chagua kulipa gharama sasa hivi au uje ulipe baadae

jacobmushi
1 Min Read
Kwenye maisha yako chochote kinachoendelea sasa hivi kilisababishwa na mambo uliyoyafanya huko nyuma.  Yawe mabaya au mazuri unahusika kwa kiasi kikubwa kwa kinachoendelea sasa.

Kama ni hivyo basi kwa chochote unachokifanya sasa kitaleta matokeo baadae jiulize unafanya nini sasa hivi na unatarajia matokeo gani baadae?  Kama unataka mambo makubwa Kwenye maisha yako anza sasa kulipia gharama. Fanya kazi kwa bidii sasa baadae utayaona matunda yake.

Watu wengi wanakwepa kulipa gharama sasa Watalipa gharama zaidi baadae una muda sasa hivi wa kufanya kitu fulani na hufanyi itakuja kukupa gharama zaidi ya kufanya kile kitu kwa haraka na kukosa ufanisi kwa maana utakua hufikiri sawa sawa.

Kama ndoto yako ni kua mtu mkuu anza kujijenga sasa hivi kwa kusoma vitabu mbalimbali vya uongozi na vya aina nyingine vinavyohitaji,  kama ni mfanyabiashara mkubwa soma sana vitabu vya biashara,  usijidanganye kua ukishakua na pesa utapata muda wa kufanya vitu fulani.

Anza sasa kidogo kidogo ni uwekezaji huo unawekeza na utakuja kukulipa usikate tamaa endelea sana kila siku ongeza thamani kwenye maisha yako.
Asante sana na Karibu
Jacob Mushi 2016
E-mail jacob@jacobmushi.com.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading