Farasi anaweza Kukimbia umbali mrefu ila hawezi Kukimbia bila mpandaji.
Mpandaji ndio atadhibiti mwendo na njia anayotakiwa apite.
Bila mpandaji huyu Farasi angeweza kupita kwenye njia zisizo sahihi. Angeweza kuvunjika Miguu kwa Kukimbia kupita kiasi.
Mpandaji akiwa mwanafunzi lazima awe na Mwalimu wake.
Huwezi kuruhusiwa kwenda porini mbali na Farasi wakati wewe bado ni mwanafunzi. Na endapo utajaribu mwenyewe unaweza kurudi na majeraha.
Kwenye Maisha maono yako, na kile unachokitaka ni sawa na Farasi. Maono hayawezi kutokea yenyewe lazima awepo mtu anaeyaendesha.
Katika kuyaendesha lazima ukubali kujifunza. Kwasababu msukumo unaweza kuwa mkubwa hadi ukazidi uwezo wako.
Unahitaji kocha wa Kukuelekeza na kukuongoza taratibu. Kuna changamoto unaweza kuzipitia sio kwasababu zilikuwa lazima Upitie bali ni kwasababu ulikataa kuongozwa.
Kuna mahali utapata hasara kwasababu hukutaka kusikiliza. Ungefuata maelekezo usikwama.
Ungekubali kukaa chini ya mtu akakuongoza ungefika mbali zaidi ya hapo ulipo.
Kila mmoja wetu anaweza kufikia Ndoto Yake. Ukiwa chini ya kiongozi mzuri utaweza kufika kwa haraka.
Usikubali kwenda peke yako katika njia mpya na hujajua vizuri kumwendesha Farasi. Atakuangusha na kukuvunja Miguu.
Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi.