Habari za siku ya leo ni matumaini yangu kwamba unaendelea mbele vyema. Leo tunakwenda kuiona hasira ambayo inaleta mabadiliko katika maisha yetu. Kila kitu kilichopo ndani yetu kinaweza kutumika vizuri kikabadilisha maisha yetu au kikatumika vibaya kikaharibu maisha yetu. Tukiweza kujifunza vyema vitu hivi vitaweza kutusaidia sana katika kuleta mabadiliko.
Kua na huzuni juu ya hali mbaya unayopitia sasa ni kupoteza muda jaribu kua na hasira na uamue kubadilisha. Huna haja ya kua na hasira juu ya watu wanaokuuzi au kukufanyia mabaya, jaribu kua na hasira juu ya hali inayokufanya uonekane wa kawaida na uibadilishe.
Ndoto zako utaweza kuzitimiza tu pale utakapokua na hasira juu ya hali uliyonayo sasa. Chochote unachokichukia kwenye maisha yako ya sasa kitaondoka tu pale utakapokua na hasira za kutosha za kukiondoa, iwe ni umaskini, ukosefu wa pesa za kutosha na kadhalika.
Hakikisha hasira ambazo ziko juu mara nyingi ni za kukufanya wewe upige hatua moja kwenda nyingine, kinyume na hapo hasira nyingine zitakua zinakuletea matatizo Zaidi na kukufanya urudi nyuma.
Mpenzi wako amekuacha kisa huna pesa ukiwa na hasira za kuachwa ukapanga kumfanyia kitu kibaya maisha yako yataharibika kabisa, lakini ukiwa na hasira za kuchukia kukosa pesa na ukazitumia hasira hizo kufanya kazi kiwa bidi hadi ufike kule unakotaka utaona mabadiliko makubwa
Daudi aliweza kumuua Goliati kwasababu alikua na hasira, alikua na hasira sana na akachukia aliposikia jina la Mungu wake linatukanwa na mtu asiyetahiriwa. Hasira zile zikamfanya aamue kwenda kupambana na Goliati bila kujali ukubwa wake, matokeo yake tumeona alimshinda adui yake.
Mtu ambaye ana hasira ni yule ambaye hataki kua katika hali ile aliyoizoea, anataka kupiga hatua ya mbele Zaidi ya mabadiliko.
Karibu sana.
Jacob Mushi