Wewe Sio wa kwanza hapa duniani hivyo ni vyema sana kuangalia wengine walifanya nini na ujifunze kwao. Hapo ulipofika hujafika kwa nguvu zako mwenyewe kuna watu walishiriki kukufikisha hapo. Haijalishi wewe ni mtu mkuu kiasi gani umekuwa tajiri kiasi gani watu wengi wamehusika kukufikisha hapo.

Kama umefika mahali ukaanza kuona hakuna anaeweza kukushauri basi umejiona umefika sehemu ya juu kuliko wengine. Tatizo linakuja pale kwamba sio wewe peke yako umejifikisha hapo ulipo hivyo waliokufikisha wakiamua kukuacha utaanguka tu.
Wewe ni mfanyabiashara unauza bidhaa zako kwa watu. Umetumia nguvu nyingi kujitangaza umejulikana kila mahali na watu wanatumia bidhaa zako. Ukijisahau ukafikiri ni nguvu zako zimekufikisha ulipo au ni bidii zako utakuwa unakosea sana. Kama wanaonunua bidhaa zako wasingefanya maamuzi ya kununua bidii yako matangazo yako yangekuwa ni bure.
Chochote unachotaka kukifanya jifunze kwanza wengine walifanyaje. Chochote unachotaka kuongea tafakari kwanza ujue kinakwenda kuleta madhara gani. Neno moja linaweza kuwa sababu ya watu wote wasikuamini kabisa. Sentensi ndogo ya dharau inaweza kufanya bidhaa zako zisinunulike tena.
Kama ulisahau nilishakwambia tena kila mmoja ni mfanyabiashara kila mmoja kuna kitu anafanya ili aingize kipato hivyo haijalishi unafanya nini hata kama umeajiriwa kuna kitu unauza ni muhimu ukajua wateja wako ni wapi.
Wewe sio wa kwanza kukosea pia lakini isiwe sababu ya kujitetea wakati ulijua unatenda kosa na ukalifanya kwa makusudi.
Kuna mambo mapya yanakuja kila siku lakini sio sababu ya kutufanya tuyadharau yale ya kwanza.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading