HATUA YA 105: Huruma ya Mteja.

jacobmushi
2 Min Read
Wewe umeanzisha biashara yako ili utatue matatizo ya watu. Ukweli ni kwamba unatatua matatizo ya wengine ili utatue na matatizo yako.
Utakuwa unakosea sana kama utakuwa unataka huruma ya mteja kwa kuharibu kazi yake au kumcheleweshea.
Mteja atakuona wewe ni mzembe na wala hujali pesa yake unajali zaidi matatizo yako.
Nilishawahi kupeleka nguo kwa fundi, nikamuuliza utaweza kufanya hii kazi? Akanijibu ndio! Nikamuonya kabisa angalia usije kuniharibia kazi yangu.
Baada ya siku tulizokubaliana nikaifata kazi yangu. Kutazama nguo yangu fundi ameharibu. Kumweleza anakuja juu na kuwa mkali. Nilipoamua kuwa mkali zaidi na kumweleze atanilipa nguo yangu akaanza kuomba tusaidiane. Yaani tugawane gharama hali ni ngumu.
Yaani kazi yangu ameharibu yeye halafu gharama ya kurekebisha nilipie tena. Haijalishi fundi huyu ana shida kweli au lah! Moja kwa moja ameshanipoteza mimi kama mteja.

Anaonekana hajali mteja wala hajali pesa yangu.
Kama unafanya biashara watu wanatafuta pesa zao kwa shida pengine zaidi yako wewe uliekaa hapo kwenye biashara. Mtu anapoleta pesa yake kwa ajili ya huduma fulani hakikisha unamhudumia sawasawa. Ukiharibu kazi ya mtu hakikisha unawajibika.
Usikimbie majukumu yako. Kama ulifanya uzembe wajibika kwa uzembe wako. Hakuna mtu anapenda kutoa pesa sehemu ambayo pesa yake haithaminiwi.
Mteja ndio kila kitu kwenye biashara yako. Mteja ndiye anaweza kuwa sababu ya wewe kupata wateja zaidi au kukuharibia kazi. Mteja akipata usumbufu kwenye biashara yako hawezi kuwaelekeza watu waje.
Usitegemee huruma ya mteja kwenye makosa yako mwenyewe. Wajibika.
Karibu sana.
Nunua Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo Wasailiana nami kwa 0654726668
Jacob Mushi
Author & Entrepreneur
Phone: 0654726668
E-mail: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading