Wakati mwingine unaweza kuogopa watu juu ya kile unachotaka kukifanya kumbe woga huo hauna maana yeyote. Hakuna mtu mwingine atakaejali au anaejali kama unavyodhani.

 

Kila mtu ana mambo yake anafanya hivyo kama wewe unapoteza muda kuwaza watu watakuonaje endelea kuchezea muda wako.
Hivi ukipata hasara kwenye biashara yako nani anajali?
Ukifeli kwenye kile ulichokianza nani anajali?
Hakuna atakaejali Zaidi yako wewe hata kama watajitokeza watakaokupa pole na kukutia moyo lakini wewe pekee ndie unatakiwa ulipe uzito jambo lako. Hakuna ambaye anakaa anafikiria kuhusu wewe kuliko wewe unavyotakiwa kufikiri.
Kama ukiona wewe hujali mambo yako basi ujue hakuna anaejali kabisa. Amua leo kuanza hao unaodhani wanakutazama hawapo. Ni picha ambayo umejijengea ndani yako lakini haina uhalisia.
Soma: Kukosea Na Changamoto
Nilikuja kugundua kwamba wakati mwingine wale tunaosubiri watuambie tunaweza kumbe na wao wanasubiri tufanye kitu.
Ili uonekane lazima uanze kufanya kitu. Hakuna anaekuhurumia kila mmoja ana Maisha yake anapambana yasonge mbele. Kikubwa ambacho unaweza kukipata kwa wengine ni ushauri na kutiwa moyo basi.
Ukitaka kujua hakuna anaejali kuhusu wewe anzisha mchango kidogo wa mtaji kwa ajili ya biashara unayotaka kuanza watu wachache sana watajitokeza. Lakini linapotokea suala ambalo wachangiaji watahusika moja kwa moja lazima watajitokeza wengi watakaokuchangia.
Hapo unagundua kwamba wengi wanajali Zaidi kile ambacho watashiriki. Wakati wa furaha na shangwe wanajitokeza wengi. Lakini wakati wa kupanda mbegu walio karibu yako ni wachache sana.
Nakutia moyo usiogope hao unaowaogopa hawapo.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading