Una nguvu kubwa sana ndani yako. Inawezekana hujawahi kuambiwa hata siku moja. Leo ninakwambia ipo nguvu ndani yako ya kushinda yote ambayo unayapitia sasa.
Ipo ngvuvu ndani yako ya kukuwezesha kufikia yale yote unayoyataka. Haijalishi sasa hivi unaona giza. Au unapitia magumu kiasi gani. Tumia uwezo ulio ndani yako kuzishinda changamoto unazopitia sasa.
Una nguvu ndani yako usiogope lolote unalopitia umebeba suluhisho. Umebeba suluhu ya matatizo yako pamoja na ya wengine. Asikuambie mtu mwingine kwamba wewe huwezi au ulishashindwa kipindi Fulani.
Usiangalie uliwahi kushindwa wapi. Hatupimwi kwa tulivyokosea au tulivyoshindwa tunapimwa kwa yale tuliyoweza kuyakamilisha. Na hata kama unafikiri wewe hujawahi kufanya chochote cha maana huu ni wakati wako. Ndio maana napenda kusema upo hai kwasababu maalumu. Kuna siri ya wewe kuwa hai leo. Maana yake ni kwamba kuna jambo bado hujafanya.
Nguvu uliyonayo ni Zaidi ya kitu chochote ulichowahi kuambiwa kasoro Mungu peke yake. Wengi wetu tukiwa wadogo tulikua tunaelezwa jinsi Wanyama wa porini walivyo na nguvu kama simba, tembo na wengineo lakini ni wachache tuliambiwa uwezo na nguvu tuliyonayo ndani yetu.
Leo mimi nakwambia una nguvu kuu sana ndani yako. Igundue nguvu hiyo uanze kufanya mambo makubwa.
Utagunduaje nguvu?
Angalia ni kitu gani ambacho unaweza kukifanya vizuri sana kuliko vingine. Kifanye kitu hicho na fikiria kwa undani Zaidi ili uweke ubora wa hali ya juu. Unajua sio kila mchezaji anaweza kuwa golikipa japo wote wapo uwanjani. Kila mmoja ana sehemu yake anayofanya vizuri. Hivyo hata wewe haijalishi unafanya kitu gani kuna sehemu upo vizuri Zaidi. Embu fanyia kazi hiyo sehemu kwani ndio inakwenda kukutoa.
Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading