HATUA YA 144: Tabia Hizi zinakunyima Mafanikio..

By | May 8, 2017
Sijawahi Kuona Tajiri mlevi hata siku moja, yaani anaelewa hadi anasahau viatu? Sijawahi kuona tajiri ambaye ana tabia za kushinda baa akilewa.
Kama unakumbuka ukiwa mdogo mar azote mtoto mwenye tabia nzuri ndiye alikua anapendelewa kwenye kila sekta. Mtoto kwenye tabia nzuri alikuwa anapewa chakula kingi kuliko wenzake. Hata katika Maisha ya sasa tabia zako zinaamua upate nini kwenye Maisha yako. Tabia zako zinaamua uambatane na watu wa aina gani.
Fursa nzuri zinapokuja kutokana na tabia zako kuna watu wanaogopa kukushirikisha. Wengine wanaogopa utawaaibisha, wengine wanaogopa unaweza kwenda kuonyesha tabia zako mbovu mbovu kule ugenini.
Kabla hujalalamika mbona mimi sipati hiki na hiki anza kuangalia tabia zako zikoje. Zinavutia watu wazuri kukaa karibu na wewe? Je tabia zako zinawafanya watu wema watamani kufanya kazi na wewe?
Anza leo kubadilika. Unaweza kuwa na ujuzi na vitu vingi vizuri lakini tabia zako zinakukosesha mengi sana. Inawezekana unafanya kazi kwa bidii sana na unapata pesa lakini ulevi na starehe zimekusonga. Inawezekana unapokea pesa nzuri sana kuliko wengine wenye mafanikio lakini wewe tabia zako zinakurudisha nyuma.
 Asilimia kubwa ya matatizo mengi tuliyonayo yanasababishwa na tabia tulizonazo kwenye Maisha yetu kila siku. Tabia ulizonazo ndio zinakufanya uwe kwenye hali uliyonayo sasa hivi. Haijalishi ni hali ya namna gani wewe angalia utakuta tabia zako zinahusika kwa kiasi kikubwa.
Hakikisha umeujua udhaifu wako uko wapi kisha amua namna njema ya kupambana na hiyo hali.
Jipatie Nakala ya Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo, Wasiliana nami kwa 0654726668.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *